Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani Philiberto Sanga ameipongeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kufuatia kuwafanyia upendeleo katika Wilaya hiyo katika kuhakikisha wananchi wanaboresha maisha yao kupitia ufugaji wa kisasa badala ya kutegemea zao moja tuu la Korosho.
Akizungumza katika hafya hiyo ya kukabidhiwa Mbuzi wa Maziwa mwishoni mwa wiki katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Sanga alimpongezsa Mbunge na Naibu Waziri wa Mifugio na Uvuvi Abdallah Ulega kwa msukumo wake kupitia semina mbalimbali za ufugaji wa kuku kwa akina mama, watendaji Kata na Walimu, hali itakayochochea kuongezeka kipato na kuboresha afya.
Sanga alimwagiza Afisa mifugo wa Halmashauri ya Wilaya, Honorius Mgunda ahakikishe anawasimamia wataalam wake ngazi ya Vijiji na Kata kuwa waelimishe Wafugaji na kutokomeza magonjwa ya mifugo sambamba na kutunza takwimu hatimaye kituo cha utafiti wa Mifugo hapa nchini (TALIRI) kiwe na kumbukumbu nzuri.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa utafiti kutoka (TALIRI) Dk, Eligy Shirima alisema utoaji huo wa Mbuzi wa Maziwa ni Mpango wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuboresha maisha ya Wananchi kupitia sekta ya Mifugo huku akitoa angalizo kuwa Mbuzi hao wametokana na fedha za Serikali ambazo zinatakiwa kuleta matokeo chanya.
Akitoa neno la shukrani Mfugaji maarufu kutoka Kijiji cha Magoza Abdallah Mokiwa amesema kushiriki kwake Maonesho mbalimbali ya Kilimo kumempa mwanga wa kujikita zaidi katika ufugaji wa kisasa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.