Naibu Waziri Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Mwita Waitara ameliagiza Baraza laTaifa Hifadhi na Mazingira (NEMC) kuhakikisha utendaji kazi wao unawashirikisha Wakuu wa Wilaya ili kuondoa migogoro kati ya Viwanda na wananchi .
Akizungumza na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama na wakuu wa idara wilayani Mkuranga leo Waitara ambaye pia ni Mbunge wa Tarime Vijijini alimwagiza kaimu Mkurugenzi wa (NEMC) Edger Mgila ahakikishe nakala za vyeti vya usajili wa viwanda wanapewa wakuu wa wilaya iwe rahisi kufuatiia uhalali wao.
Kiongozi huyo alimtaka Kamanda wa Polisi Wilaya (OCD) Andrew Ngassa (SACP) kufuatilia upelelezi wa kesi ya kugushi nakala ya (NEMC) ikiwemo sahihi ya aliyekuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira George Simba Chawene inayowakabili kiwanda cha Bugalo.
Aidha aliliagiza baraza hilo kufuatilia malipo kwa Wananchi wanaotakiwa kupisha kiwanda cha nondo Fujian kilichopo kisemvule ambacho moshi wake mzito una athari.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mkuranga Filberto Sanga alimwomba Naibu Waziri awasaidie kuondoa migogoro kwa kuwaagiza (NEMC) kabla ya kutoa kibali washirikiane na Wizara ya Ardhi uwekezaji ili kujiridhisha usalama wa eneo la ujenzihuku wakitoa kipaumbele kwa Halmashauri kama yao ambayp ina eneo la ardhi kwa uwekezaji.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri Wilaya Mohamed Mwela aliwataka wawekezaji ambao wanakuja kwao wasiwatumie madalali kuwaudhi ardhi badala ya idara ya ardhi Halmashauri ili kupata maeneo sahihi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.