Wajasiriamali wilayani Mkuranga wamepatiwa Kuku zaidi ya 1000, kama mtaji ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokona na umaskini.
Akipokea Kuku hao hapo jana kutoka kwa kampuni ya AKM greeter iliyoahidi kutoa Kuku 4000,Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh Filberto Sangaamewataka wakina mama wote watakao nufaika na Kuku hao wasitumie kwa kitoweo bali wafuge ili waweze kuinua vipato vyao vya familia zao.
Aidha Sanga amesema kuwa matarajio yao baada ya mwaka mmoja wakina mama hao hawatakuwa na hali walizonazo sasa."watanufaika katika mambo mengi sana,moja wapo watapata mayai ambayo watauza na Kuku wakizaliana watauza na kuongeza kipato cha familia"alisema
Sanga aliongeza kwamba kina mama wa Mkuranga wanabahati sana kuliko wenzao kwa hiyo watumie nafasi hiyo kwa ajili ya kujinufaisha."Mbunge ulega anafanya kazi nzuri sana na nampongeza,kina mama msimwangushe"alisema sanga
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde amesema jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi wilayani Mkuranga liliendesha mafunzo ya siku mbili kwa wajasiriamali walijifunza,jinsi ya kutunza fedha na kufanya biashara kwa tija,ambapo katika mafunzo hayo wajasiriamali hao waliahidiwa kupewa Kuku 4000 ili wafuge kwa ajili ya kujikimu kiuchumi na kuondokana na umaskini,ambapo kwa awamu ya kwanza wamekuja Kuku 1058 waliogaiwa kwa wajasiriamali 100 kwa kila mmoja Kuku kumi.
Aidha Munde amewataka kinamama hao kwenda kutumia utaalam waliopewa kwenda kutoa elimu kwa wengine na kuleta tija kwa taifa kwa kujiongezea kipato chao na familia
"Kwenye mafunzo waliambiwa Kuku waliopewa sio zawadi,kuku wale wamepewa ili waweze kuwafuga na kuzalisha kwa hiyo maana yake wamepewa Kuku kumi lakini baada ya muda watatakiwa wawe na Kuku zaidi."alisema Munde
Munde alisisitiza kwamba wana imani sana na wale wote waliopata Kuku watawaendeleza na kuleta matokeo chanya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa jukwa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilayani Mkuranga bi Mariamu ulega aliwashauri wakina mama wa Mkuranga kutumia Kuku hao kama chachu ya maendeleo ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ya hapa kazi tu na kuifanya Tanzania ya viwanda."kina mama tuamke kama Mh.Rais anavyosema tulete Tanzania mpya,tutoke majumbani hakuna kitu kitakacho tukomboa zaidi ya kufanya kazi. "Alisema Mariamu
Kwa upande mmoja wa wajasiriamali waliokabidhiwa Kuku hao bi. Sauda Pazi alisema wanamshukuru Mbunge wa Jimbo
La Mkuranga Mh Abdalah ulega, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Mkuu wa Wilaya pamoja na Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake kwa msaada huo,ambao alisema watautumia vizuri katika kujikwamua kiuchumi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.