Wakati Rais wa jamuhuri ya Muunganao wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiendelea kuwahakikisha wakulima wa zao la korosho kupata soko kwa bei ya zaidi ya shilingi 3000 kwa kilo moja ikiwa wanunuzi wa zao hilo hawatajitokeza katika mikoa inayolima zao la korosho, wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani imeanza kusambaza magunia ya kuhifadhia zao hilo kwa wakulima kupitia vyama vya msingi-AMCOS
Ofisi ya Habari ilimefika katika moja ya ghala linalokusanya zao la korosho kwa hatua ya awali kabla ya kuzipeleka katika ghala kuu lililochaguliwa na wilaya hiyo kwa ajili ya kufanyika mnada na kushudia baadhi wa wakulima wakigawiwa magunia hayo ili waweze kuhifadhi kwa utaratibu unaostahili wa zao la korosho baada ya kukaguliwa katika ubora tofauti.
Wakizungumza baadhi ya wakulima wa zao la korosho waliofikisha bidhaa hiyo katika ghala la chama cha ushirika mkuranga -AMCOS na kukaguliwa korosho zao ikiwa ni pamoja na kupewa magunia ili waweze kuhifadhi kwa utaratibu unaostahili walisema.
Mwenyekiti wa chama cha msingi wilaya ya mkuranga-AMCOS Twaha Ramadhani ameelezea jinsi wanavyopokea korosho katika ghala hilo kabla ya kuepeleka katika ghala kuu.”tunakagua ubora wa korosho tunatoa mbovu na kubakisha nzima na pia tunakagua ukavu wa korosho na baada ya hapo tunampa gunia ya kuweka korosho”Ramadhani alisema
Naye afisa ushirika wilaya ya Mkuranga Lawi Magoko alisema idadi ya magunia yaliypokewa ni robota 323 na tayari wameshaanza kusambaza kwenye vyama vya ushirika na zimebaki robota 21 za ziada na robota 300 zinatarajia kuja muda wowote.
Pamoja na hilo Serikali imesema wameshapata wanunuzi kwa ajili ya zao la korosho kwa bei ya shilingi 3,300 kwa kilo moja.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.