Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga ameshiriki katika kufunga mafunzo ya Warsha ya Jamii (Community session) ambayo yamefanyika siku tatu katika ukumbi wa mkutano ndani ya Jengo la Halmashauri.
Lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo wawezeshaji ili watumie nyenzo hizo za kutoa elimu kwa wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini (TASAF) ili waweze kutumia Ruzuku wanazopokea kwa lengo lililokusudiwa la kuboresha maisha yao.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya MKuranga Bi. Mwantum Mgonja amemshukuru Bw.Ladislaus Mwamanga Mkurugenzi wa TASAF kwa kuridhia mafunzo hayo yafanyike Mkuranga.
Aidha bi. Mwantum amewataka wawezeshaji kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha walengwa wote wa TASAF wanafikiwa kwa wakati na kupewa huduma stahiki.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.