Mratibu wa mradi wa kusaidia kaya masikini (TASAF) Mkoa wa Pwani bi Asha Itelewe amewataka wazazi ambao ni wanufaika wa mradi huo kuipa elimu kipaumbele kwa kuwapeleka watoto wao shule ili watoto waje kuwa msaada kwa wazazi wao lakini pia iwe sehemu ya kujikomboa kielimu na maisha kwa ujumla
Akizungumza katika ziara iliyofanyika katika kijiji cha kisemvule na vikindu vilivyopo katika Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani bi Itewele alisema wakati tuliopo ni wakati ambao unahitaji wasomi wengi katika jamii ili kuwezesha mambo mbali mbali ya maendeleo kupiga hatua hivyo basi
“Nitoe rai kwa wanufaika wote kuwapeleka vijana shule kwani kwa kufanya hivyo kama mzazi au mlezi utakua umempa mtoto haki ya kupata elimu lakini pia umemsaidia kufuta ujinga sambamba na kumuongezea uelewa na atajua kadri anavyokua afanye nini ili kukabiliana na hali ya umasikini katika jamii yake”
nae Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Bi Jessy Mpangala aliongezea kwa kusema Serikali yetu tukufu inatoa elimu bure kwa lengo la kumfanya kila mtoto mwenye umri wa kuanza shule apate fursa ya kuitumia haki yake bila vikwazo vyovyote hivyo wazazi na walezi fedha inayotengwa kwa ajili ya kununua mahitaji ya mwanafunzi ifanye kazi hiyo sawa na malengo ili kupunguza ghasia za kumkosesha mtoto vitu muhimu ikiwemo sare za shule kwa kutumia fedha iliyotengwa kwa matumizi mengine.
aidha Afisa lishe Wilaya Bi Vumilia Mbughi alisisitiza ulaji wa mlo kamili ili kusaidia ukuaji wa afya ya mwili na akili kwa watoto na familia nzima, lakini pia amewataka wanufaika wa mradi wa tasaf kulima bustani za mboga mboga ili ziweze kutumika kama sehemu ya mlo wao wa kila siku na watoto wasinyimwe vyakula muhimu kwa kuwapa baba zao.
Takribani Milioni 156 zimetolewa kwa kaya masikini 3420 katika vijiji 75 vilivyoo ndani ya halmashauri ya wilaya ya mkuranga.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.