Walimu wa Halmashauri ya Wilaya Mkuranga Mkoa wa Pwani waonywa kuepuka tamaa ya kupoke hela kwa ajili ya kuvunja miiko ya kusimamia mitihani ya darasa la saba
Akizungumza na walimu na wasimamizi watakaoshiriki katika kusimamia mitihani hiyo, kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kanyala Mahinda ambaye amemuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji aliwataka wasimamizi wawe makini na watimize wajibu wao kulingana na sheria na taratibu za utumishi wa umma kama zinavyowataka katika zoezi zima la usimamizi wa mitihani .
Aidha Kaimu Mkurugenzi mtendaji alisema, mitihani ya darasa la saba ni zoezi maalumu na ni kazi ya siri, lakini pia aliwaasa kama watasimamia vizuri matokeo yatakua mazuri na kama itasimamiwa vibaya matokeo yake yanaweza kuwa mabaya na athari zinaweza kuanzia kwa msimamizi wa mtihani kwani zipo sheria zinazosimamia watu wote wanaokiuka taratibu za kusimamia mitihani.k
Kwa upande wake Afisa Elimu msingi wilaya ya Mkuranga Cosmas Magigi alimuhakikishia mkurugenzi kutekeleza maagizo yote huku akitaja idadi ya wanafunzi wataofanya mitihani ni 6673 ambapo wasichana ni 3493 na wavulana 3180.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.