Mkuu wa mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo ameagiza jeshi la Polisi Mkoa kuwakamata viongozi wa Vikundi 10 vya usimamizi wa Korosho vilivyofanya udanganyifu kwa wanunuzi wa korosho. Kauli hiyo aliitoa katika kikao maalumu na viongozi wa wilaya na wadau wa Korosho tarehe 28.12.2017 wilayani Mkuranga.
Alisema, ' vyama vya msingi vilivyofanya udanganyifu kwa kuweka mchanga na kokoto katika Korosho, viongozi wao yaani Mwenyekiti, Katibu, Karani na Mtunza ghala wakamatwe na kuhojiwa kisha kufunguliwa jalada la uchunguzi ili kuweza kuwabaini wote waliohusika katika udanganyifu huo.
Aidha ametangaza kuwa msimu wa korosho kwa mwaka 2018 Korosho yote ya Mkoa wa Pwani itahifadhiwa katika maghala makuu 3 tu ambayo yatakuwa Kibiti, Mkuranga na Kibaha kwa Mfipa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.