Wanafunzi 20 waliokatishwa masomo yao kwa kupata ujauzito kwa bahati mbaya wamerudi shule kuendelea na masomo yao wilayani Mkuranga mkoani Pwani baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza wanafunzi hao warudi shule kuendelea na masomo yao.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ally katika maadhimisho ya siku ya mwanamke kiwilaya katika viwanja vya shule ya msingi Mkuranga
Amesema kwa taarifa alizonazo wasichana hao 20 walikwishajifungua waliomaliza kunyonyesha watoto wao sasa wamerejea shuleni.
Khadija alisema hiyo sio taarifa nzuri lakini ni taarifa nzuri, ni taarifa nzuri kwasababu pale walipoona giza kuendelea na ndoto zao lakini sasa wanaendelea na ndoto zao kwa kurekebisha makosa yao waliyofanya.
"Ni taarifa nzuri kwasababu unapojikwaa na kuanguka unapoinuka hautainuka na mguu ule ule uliojikwaa yaani wadogo zetu waliojikwaa na kupata ujauzito sasa wataenda kufanya vizuri na kuwa mfano kwa wengine" alisema Khadija.
Aidha aliwataka Walimu kuwasaidia wasichana waliopata changamoto za namna hiyo kwasababu kikawaida kisaikolojia wasichana hao hawawezi kuwa sawa na wasichana wengine.
"Na ndio maana tumewawekea utaratibu wa kupata elimu ya watu wazima na tusiwaache kwasababu wazazi wao peke yao hawataweza kusimamia maendeleo ya wasichana hao bila sisi serikali, Walimu pamoja na Walezi kushirikiana kwa pamoja" alisema.
Hatahivyo Mkuu huyo wa Wilaya ya Mkuranga alionesha kukerwa na baadhi ya wazazi ambao watoto wao wamefaulu darasa la saba lakini hadi sasa bado hawajaripoti shuleni kuendelea na masomo yao na sekondari.
Khadija alisema serikali imefanya jitihada kubwa kujenga madarasa na kuhimalisha miundombinu ya elimu wilayani humo kwa gharama kubwa kubaki nyumbani na wanafunzi hao ni kutojali na kutothamini jitihada hizo za serikali.
Alisema atawaita wazazi hao kwa kufanya mkutano nao ili kuwasikiliza ili kujua sababu za wanafunzi hao kutoripoti shule na baada ya hapo iwapo bado kutakuwa na wasioripoti tena shuleni hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Meneja wa Bank ya CRDB tawi la Mkuranga Martha Ngowi akizungumzia akaunti mpya ya Malkia kwa wanawake ambayo bank hiyo wameianzisha kwaajili ya kuwasaidia wanawake kuhifadhi fedha zao badala ya kuhifadhi kwenye vibubu majumbani njia ambayo sio salama kwa utunzaji fedha.
Naye Afisa Maendeleo ya jamii wilaya ya Mkuranga Amina Hoja alisema bado jamii kubwa ya wana Mkuranga wanatekeleza mila ya mwanamke kukaa na kusubiri kuletewa kwa mtazamo wa kuwa mume ndiye anapaswa kuhudumia familia peke yake.
Amina alisema uelimishaji unaendelea kufanyika ili kubadili fikra za jamii hiyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.