Wanafunzi waliofauli vizuri wapewa Karo ya Shule.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mh Juma Abeid Leo ametekeleza ahadi ya kutoa karo kwa wanafunzi watano wa Sekondari ya Tengelea waliofanya vizuri kwenye Elimu ya kidato cha nne.
Abeid alisema"Nimefarijika sana kwakua vijana hawa niliwapa ahadi ya kuwa endapo wakipata daraja la kwanza hadi la pili nitawalipia karo na leo nina furaha kwamba Vijana hao watano wamefaulu vizuri kwa kupata daraja la pili".
Abeid aliongeza kwamba ni wajibu wa viongozi kuwaunga mkono wanafunzi wanaofanya vizuri ili kuwapa motisha na wengine waweze kufanya vizuri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Eng.Mshamu Munde alisema katika ukanda Pwani kuna hali ya Elimu kuwa chini lakini kutokana na motisha na hamasa wanayotoa inasaidia wanafunzi kufanya vizuri.
Munde alisisitiza kwamba Serikali imeleta vifaa kama vitabu na vifaa vya maabara kwa lengo la kuhakikisha wanafunzi wanapata Elimu bora.
Mwanafunzi Mustafa Abdallah kutoka Sekondari ya Tengelea ni mmoja wa wanafunzi aliyefaulu na kupata karo alisema"Nashukuru Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga,Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi Mtendaji kwa kuona umuhimu wa kutusaidia karo ya shule."
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga pamoja na viongozi wake wamekuwa mstari wa mbele kwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Pombe Magufuli kwa kutoa motisha,hamasa na kuwatia moyo wanafunzi wanaofanya vizuri ili wengine wapate hamasa ya kusoma kwa bidii na kufanya vizuri.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.