Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bwana Cosmas Magigi ambaye pia ni Afisa Elimu Msingi amewataka wanafunzi kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu.
Magigi aliyasema hayo hapo jana kwenye hafla fupi ya kukabidhiwa vitabu na Taasisi ya Hakielimu iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Kiparang’anda.
“Hakielimu imekua ikiangalia changamoto za serikali na kuzifanyia kazi,tunashukuru na wao wamechukua hatua kwa kuona uhaba wa vitabu katika shule zetu na kutuletea”. Magigi alisema
Magigi aliongeza kwamba walimu wamekua wakiwaandaa wanafunzi kujibu mitihani na baada ya kumaliza mitihani hiyo wanaacha kujisomea na kusababisha mwanafunzi kukosa ujuzi katika maisha.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Hakielimu Bwana Robert Mihayo alisema lengo la kugawa vitabu hivyo ni kuunga mkono juhudi za serikali kusaidia upatikanaji wa vitabu katika shule zake nchini na pia zoezi hili lina lengo la kuhimiza tabia ya kusoma vitabu miongoni mwa watanzania wa marika yote.
“ingawa vitabu hivi si vya kiada tunaamini kuwa vitasaidia kuimarisha uelewa wa wanafunzi na wananchi wote kwa ujumla kuhusu masuala mbalimbali,pia zoezi hili linataka kujenga utamaduni wa kupenda kusoma miongoni mwa watanzania ambayo iko chini sana”Mihayo alisema
Mihayo aliongeza kwamba ni muhimu watanzania kujenga utamaduni wa kusoma vitabu ili kuchota maarifa mbalimbali na kuwasaidia katika kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Rehema Ngelekele Mwenyekiti wa kujitolea katika masuala ya elimu kwa kushirikiana na Hakielimu kanda ya kusini alisema alifanya uchunguzi kwa baadhi ya shule za Msingi na Sekondari na kuona upungufu wa vitabu vya ziada na kuchukua hatua kwa kuwaomba Hakielimu waweze kusaidia.
Hamidu Ningoningo mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Kiparang’anda alisema ”Naishukuru sana Taasisi ya Hakielimu kwa kutuwezesha vitabu vya ziada kwani tulikuwa na upungufu mkubwa na vitabu hivi vitatusaidia kupata maarifa na kupandisha ufauu wetu”
Neema Simon Mwanafunzi wa kidato cha Tatu alisema vitab
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.