Wilaya ya Mkuranga imehamasishwa ulimaji wa zao la Viazi lishe kwa lengo la kuboresha afya na kufanya biashara. Hayo yalisemwa hapo juzi na bi Marry Yongolo ambaye ni mtafiti wa mazao ya mizizi kutoka katika kituo cha utafiti kibaha wakati wa zoezi la uvunaji wa mbegu za viazi kutoka kwenye shamba darasa katika kijiji cha Mikere kata ya Njia nne wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Bi Yongolo alisema Viazilishe husaidia upatikana wa vitamin A hasa kwa watoto chini ya miaka miwili na huondoa udumavu,husaidia ubongo kukua vizuri,hupunguza saratani za utumbo kwakua hufanya mmeng’enyo wa chakula kwenda vizuri.
Afisa kilimo kijiji cha Mikere bi Lydia Ungado alisema wakulima wameupokea mradi wa Viazi vizuri kwani wamefaidika na ulimaji wa viazilishe na wananchi wanapata faida kwa kutumia majani yake kama mboga pamoja na viazi kama chakula na kuuza.
Viazi vitamu ni moja ya mazao muhimu ya chakula na biashara kote nchini,hutumika kwa chakula na watu wa umri ama rika zote.Viazi vitamu ni mojawapo ya mazo ya mizizi na ni zao la pili kwa umuhimu baada ya muhogo.Pia ni zao ambalo linakomaa kwa muda mfupi kulinganisha na muhogo. Viazi lishe na majani yake ni vyanzo vikuu vya wanga, vitamin na madini.Viazi vyenye rangi ya chungwa ndio vina vitamin A kwa wingi.
Mpaka sasa mradi huu umetoa mbegu kwa kaya 3200 na
umeshirikisha vijiji vya Mikere,Kiwambo,Bigwa,Kise,Hoyoyo,Tengelea, Miteza,Lukanga, Kilamba, Lupondo, Kizomla, Mbuyuni, Kilimahewa,Dondweoza na Magoza.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.