Kamati ya Siasa Mkoa wa Pwani sambamba na kamati ya Siasa Wilaya ya Mkuranga leo Septemba 11, imefanya ziara ya kukagua mradi wa maji katika kijiji cha mwanambaya kilichopo Kata ya Mipeko
katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema jumla ya shilingi bilioni 314 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji Mkoani humo.
Akiendelea Mkuu wa Mkoa alibainisha mpaka sasa tayari DAWASA na RUWASA wameshatekeleza miradi ya upatikanaji wa maji na kuwafikia wananchi kwa wastani wa asilimia 78.
Mwenyekiti ya kamati ya siasa Mkoa wa Pwani Ramadhani maneno amewaomba wananchi kutunza miundo mbinu ya maji, kulipa gharama za uendeshaji kwa wakati ili pindi inapotekeo matengenezo ya miundo mbinu yafanyike kwa haraka.
Akisoma taarifa kaimu meneja wa maji vijini RUWASA Maria Malale lisema mradi wa maji katika Kijiji cha mwanambaya ulianza kutekelezwa julai 2018 na miundo mbinu ya mradi huo inatarajiwa kusambazwa kwa umbali wa Km 39 na gharama zilizotumika ni kiasi cha shilingi bilioni 2.3
Meneja huyo alisema, mradi huu unakadiriwa kuhudumia kaya 800 na mpaka sasa maombi ya kaya yaliyopokelewa kwa ajili ya kuunganishiwa maji ni 71 kati ya hizo tayari kaya 21 zimeshaunganishwa na zinatumia huduma hiyo.
Akibainisha Changamoto Diwani wa Kata ya Mipeko Mh. Adili Kinyenga alisema kuna wananchi wanaunganishiwa maji kwa gharama kubwa hivyo amewaomba watumishi wa DAWASA kurudi ofisi za Kijiji na kata na kujadili namna ya kuziendea gharama hizo bila kuathiri watumiaji wa huduma ya maji.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.