Serikali imewahakikishia wanawake wanaoishi vijijini kwa itaendelea kuboresha maisha yao kwa kuwawezesha mikopo kupitia halmashauri za wilaya na miji kupitia makusanyo yao.
akizungumza kwenye sherehe za siku ya mwanamke anayeishi kijijini ambayo kitaifa ilifanyika kwenye kijiji cha kazole wilayani mkuranga mkoa wa pwani leo15/10/2020 katibu mkuu wizara ya afya, maendeleo ya jamii,jinsia, wazee na watoto john njingu alisema wanatambua wao ni nguzo na walezi wa familia.
njingu aliongeza kuwa serikali imetenga shilingi bilioni (40) mikopo mbali mbali sekta ya kilimo na ufugaji sambamba na kujenga viwanda vidogo kupitia rasilimali za vijiji.
akifafanua zaidi kiongozi huyo alisema serikali imeanzisha wakala wa umeme vijijini (rea) na wakala wa barabara mijini na vijijini (tarura) ili umeme upatikane vijijini sambamba na barabara zipitike hatimaye kupunguza mzigo wa wanawake vijijini.
kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya mkuranga mhandisi mshamu munde alisema wanaunga mkono azimio la umoja wa mataifa kwa vitendo kwa kuwakwamua kiuchumi wanawake wa vijijini kupitia mikopo asilimia nne ya makusanyo yao ya ndani huku akitaja mwaka jana wametoa mikopo kwa wajasiliamali sh. milioni (500) huku mwaka huu wakitenga milioni (700) na tayari wametoa mil. (130).
kwa upande wake mwakilishi wa shirika la kutetea wanawake baraniafrika (wildaf) vera asenga aliwataka wanawake wa vijijini kupanua masoko ya biashara kwa kutumia mitandao ya simu kurusha bidhaa zao hatimaye watambulike kimataifa huku endapo watahitaji msaada wa kisheria wataupata kutoka kwao.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.