Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga amewaagiza watendaji wa kata na vijiji pamoja na wataalamu wa ngazi hizo kuishi katika vituo vyao vya kazi badala ya kuishi maeneo tofauti na wanakofanyia kazi.
Ameyasema hayo katika mkutano kazi akiwa Kijiji cha Kimanzichana na wataalamu ngazi ya kata na vijiji pamoja na viongozi mbali mbali wa ngazi hizo na kuwasisitiza kuwa watendaji na wataalamu wasiotekeleza agizo hilo waandike barua kuwa wameshindwa kufanya kazi.
Sanga akitoa maelekezo katika Mkutano huo amesema Wilaya ya Mkuranga siyo ya wafugaji bali ni ya wakulima kutokana na maeneo mengi kuonekana hayafai kwa shughuli za wafugaji na kuwataka viongozi wa vijiji kutoshiriki kuwaleta au kuwapokea wafugaji kwa kushawishiwa kwa kupewa fedha au mifugo yao.
Aidha amewataka viongozi wa vijiji kuanza kuwaondoa wafugaji wote ambao wamevamia maeneo ya mashamba ya watu na kurudishwa walikotoka na kuwaahidi kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Mkuranga itafika kuangalia utekelezaji huo.
Pia amewataka kuhakiki upya idadi ya wafugaji pamoja na mifugo yao kwa wote ambao walikubaliwa na kupokelewa kwa kufuata taratibu na ikibainika kuna ongezeko la wafugaji au mifugo yao basi wahakikishe kuwa idadi ya mifugo iliyoongezeka iondolewe pia na kubaki idadi ya mifugo iliyokubaliwa kihalali kwa mujibu wa eneo husika.
Wilaya ya Mkuranga kwa sasa imekuwa na changamoto kubwa sana ya ongezeko la mifugo ya Ng’ombe na kupelekea migogoro ndani ya vijiji kati ya wakulima na wafugaji.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.