Watendaji wa Kata 25 na wa Vijiji 125 wa Wilaya ya Mkuranga leo wamesaini Mikataba ya Kuimarisha Lishe kwa Watoto chini ya miaka 5 na Wananchi wa wilaya ya Mkuranga kwa ujumla ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi .
Mikataba hiyo imeshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bi. Khadija Nasr Ali na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndg. Mwantum Mgonja inalenga kwenda kusimamiwa kikamilifu zoezi hilo ili kuhakikisha watoto na wananchi wa Mkuranga wanakuwa na Afya Nzuri, kwani kunaonekana kuna watoto wengi wanazaliwa wakiwa hawana Afya nzuri kwa sababu wazazi wengi wanaobeba ujauzito kukosa lishe Bora.
Bi. Khadija amewataka Watendaji hao kwenda kulisimamia vizuri jambo hili kwa Miaka minne (4) iliyobaki kama tulivyofanya vizuri kwa miaka minne (4) iliyopita na kupelekea kuwa miongoni mwa Wilaya zilizofanya vizuri.
“Hili suala limepewa uzito mkubwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan, hivyo hatuna budi kwenda kulifanya jambo hili kwa uadilifu” Mkuu wa Wilaya alisema.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo amewaaambia watendaji wa Vijiji na Kata ndiyo wanahusika na wananchi moja kwa moja hivyo wanatakiwa kulichukulia jambo hili umuhimu mkubwa .
“lengo la Mikataba hii ni kufanikisha na kuboresha hali ya Lishe na kupunguza athari za utapia Mlo katika Jamii” Mkurugenzi alisisitiza.
Wilaya ya Mkuranga imefanikiwa kupunguza tatizo hili la Utapia Mlo mkali kutoka watoto 4573 mwaka 2018 hadi watoto 57 Mwezi Septemba Mwaka huu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.