Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Mhe. Filberto Sanga amewataka watendaji kata kuwa mabalozi wazuri wa elimu ya masuala ya lishe na kilimo cha viazi lishe
Sanga ameyasema hayo jana wakati akifungua mafunzo ya kilimo cha viazi Lishe wilayani hapo yaliyoandaliwa na Mradi wa ‘Sambaza Mbegu Fasta’ (Fast Track) kwenda kwa watendaji wa kata ikijumuisha madiwani, maafisa kilimo, maafisa lishe, maafisa maendeleo ya jamii pamoja na maafisa ugani
Alisema amefurahishwa na mafunzo hayo kwani yataleta tija kwa afya za wana mkuranga hususani kwa watoto ambao ndio wahanga wa ukosefu wa lishe bora, pia akagusia mipango sahihi ya kupata mtoto mwenye afya njema kuwa inaanza mapema kabla mama hajabeba ujauzito
“leo hii mmetuongezea kitu kwamba kama tunataka kufanya kazi ya uumbaji tuanze kujiandaa mwezi mmoja kabla kuhakikisha tunakuwa wazima, haya hayasemwi kwa lengo la kufurahisha ila kumsaidia Yule tuliye mkusudia kumleta duniani awe na afya njema na akili timamu “
Awali mafunzo hayo yalitanguliwa na mada kutoka kwa wataalam mbalimbali ambapo Dr.Kiddo Mtunda , Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Sambaza Mbegu Fasta kutoka kituo cha utafiti Kibaha alitoa mada juu ya Kilimo Biashara na kutoa taarifa ya mradi huku Bi. Mshugaley M. Ishika, Afisa kilimo mkuu TARI – Makao Makuu, alitoa maada juu ya chakula na lishe akisisitiza watu kula chakula chenye mchanganyiko wa makundi yote ya chakula yani protini,vitamin,wanga,mafuta na madini bila kusahau maji na fiber (nyuzinyuzi)
Aidha Bi. Vidah Mahava, alielimisha juu ya kilimo na jinsia alishauri kuwe na usawa wa kijinsia ili kumuinua mwanamke, hali ambayo inaweza kupunguza njaa katika jamii kwani wanawake wamekua wanatengwa zaidi katika shughuli zenye kipato kikubwa na kupelekea hali ngumu
Mafunzo hayo yalienda sambamba na zoezi la mafunzo kwa vitendo juu ya uzalishaji wa viazi na mbegu yaliyoratibiwa na mtafiti wa kilimo TARI – Kibaha Bi. Mary Yongolo
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo, waliipongeza serikali na taasisi hiyo kufanikisha mafunzo hayo kwani yamekua msaada mkubwa kwa kutoa elimu ya mambo ambayo walikua hawayajui ama kuwa na uelewa mdogo kwao na kuahidi kufikisha elimu hiyo kwa jamii pia “mwanzo tulikua tunajua viazi ni kwaajili ya kupika tu ila kupitia mafunzo haya nimetambua bidhaa kama keki , tambi na juice vinaweza kuzalishwa kupitia viazi lishe” alisema Bi. Salama Mhina Afisa Kilimo kata ya Beta
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.