Katika kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanapata haki sawa ya kupata elimu na kuishi katika mazingira kama wanavyoishi watoto wengine, asasi ya Kiraia ya Asma Mwinyi Foundation mwishoni mwa wiki wamegawa viti vinne kwa watoto wapatao wanne wenye uhitaji huo.
Mkurugenzi wa asasi hiyo, Asma Mwinyi akikabidhi viti hivyo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, amesema wanashukuru kwa kupewa nafasi ya kusaidia jamii ndani ya Wilaya ya Mkuranga na kusisitiza kuwa wataendelea kuwasiliana na wadau na mashirika mbalimbali ili kupata vifaa zaidi ili kuendelea kuisaidia jamii hiyo.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde amesema wilaya ya Mkuranga kwa sasa imekuwa ni kimbilio la watu wengi kutoka Mkoa wa Dar -es- salaam na kusababisha kutoa huduma za Afya kwa idadi kubwa ya wagonjwa tofauti na idadi elekezi inayotakiwa sambamba na kupokea majeruhi wengi ukizingatia Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ipo pembezoni mwa Barabara ya Kilwa.
Aidha, Munde ameishukuru asasi hiyo kwa kutambua changamoto zinazoikabili jamii ya Watoto wenye ulemavu pamoja na kuwapongeza kwa kufanikisha kuwasaidia watoto hao na kuwataka kuendela kutafuta wadau na mashirika mbalimbali kupitia wao ili kufanikisha kusaidia jamii hizo.
Viti hivyo kwa watoto hao umekuwa msaada mkubwa kwa wazazi wa watoto hao ambapo itawawezesha kufanya baadhi ya shughuli ambapo awali ilikuwa ni vigumu kufanya hivyo kwani muda mwingi walikuwa karibu na watoto wao.
Pia wazazi wametakiwa kutowaficha watoto wenye ulemavu vyumbani na badala yake wawatoe nje ili jamii iwaone na kupatiwa msaada kwani miongoni mwao kuna vipaji vingi ambavyo vitaisaidia Taifa kiujumla.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.