Watu wenye ulemavu wilaya ya Mkuranga wameuomba uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kuwaongezea bajeti ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Shirikisho la watu wenye ulemavu waliyasema hayo mwanzoni mwa wiki hii wakati walipokuwa wakizungumza na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.
Aidha wameiomba Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kuongeza asilimia mbili zaidi kwenye bajeti kwenye sehemu ya elimu ili kutatua changamoto mbalimbali zinaowakabili ikiwemo miundombinu, waalimu wataalamu na vifaa vya kujifunzia.
Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Wilaya ya Mkuranga Hassan Kambangwa alisema hivi karibuni wamekuwa na vikao mbalimbali na kamati za shule lengo kubwa kuangalia changamoto za watoto wenye ulemavu na moja ya changamoto ni kwamba hakuna ngazi mtalazo katika shule kwani majengo ni ya zamani na vyoo kwa watoto wenye ulemavu hivyo wazazi kukata tamaa kuwapeleka shule kwakua itawasumbua namna ya kujisaidia.
Mwenyekiti huyo aliongeza kwamba wamefanya utambuazi wa watoto wenye ulemavu ambao hawako shuleni na kupata idadi ya zaidi ya 200 ambao hawapo mashuleni hivyo ndio maana wanamba waongezewe bajeti kwakua bajeti ya mwanzo ilikuwa imelenga watoto waliopo mashuleni tu lakini kwa sasa wamezidi hivyo inahitajika ongezeko la fedha ili kukidhi mahitaji ya watoto hao na kuboresha miundombinu ya shule
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bwana Peter Nambunga alisema kwamba ili kuweza kuongeza bajeti ni kupata takwimu halisi ya idadi ya watu wenye ulemavu na sehemu walipo.
Nambunga aliongeza kwamba kwa Mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashari imetenga mil 60 kwa ajili ya mikopo ya watu wenye ulemavu ambapo kwa robo ya kwanza kiasi cha Tshs Mil 15 ipo mbioni kuingia kwenye akaunti za wahusika.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.