Watumishi wa umma wametakiwa kuepuka migogoro katika utendaji wa kazi na badala yake kufuata sheria na kanuni za utumishi kwa kujadiliana na muajiri ili kusaidia kuendelea kutoa huduma mbalimbali kwa jamii
Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania mkoa wa Pwani -TALGWU-Ramadhani Kinyogoli katika mkutano na watumishi wa idara ya afya wilaya ya mkuranga ukiwa na lengo la kujadilia masuala mbalimbali ya watumishi
''Wajibu na haki ni muhimu kwa watumishi ili kuhakikisha huduma mbalimbali zinazotolea katika taasisi za serikali na kuepuka migongano inayoweza kuchangia kurudisha nyuma shughuli za maendeleo hivyo watumishi hatuna budi kuepuka migogoro na badala yake kukaa meza moja na mwajiri ili kujadiliana changamoto na kushauriana.alisema
Kinyogoli
Hata hivyo Kinyogoli alibainisha kuwa watumishi wengi wana changamoto za kiutumishi ikiwa in pamoja kutOkujua sheria za kazi,kanuni na wajbu hivyo uongozi wa TALGWU Mkoa utajipanga kuendelea kutoa elimu hiyo ktika wilaya zote ili kuwasaidia watumishi hao kutambua haki zao.
''Tumebaini mambo mengi kwa watumishi
pamoja na hivyo lazima elimu hii watumishibkujiunga na vyama vya wafanyakazi ili kupata elimu hiyo na kusaidiana pale wanapopata changamoto katika utumishi".alisema Kinyogoli
Angelina Malugu ambaye ni Afisa muuguzi msaidizi wa hosptali ya wilaya ya Mkuranga alisema kuwa wanashukuru TALGWU kufika katika idara hiyo na kuzungumza na watumishi huku akibainisha changamoto za kutolipwa haki zao kwa kufanya kazi zaidi ya Masaa ya kazi pamoja na kupeleka malalamiko hayo kwa uongozi wa hosptali hivyo kuomba kushugulikiwa changamoto hizo kwa watumishi.
''Watumishi tuna changamoto nyingi tunashukuru TALGWU kufika hapa tunaomba watumishi tutatuliwe changamoto zetu maana kuna baadhi ya watumishi wanadai fedha za Masaa ya ziada ya kazi,sare za watumishi wa afya ni muda mrefu fungu hilo halitolewi" alisema Angelina Malugu
Naye Regina Kombo ambaye ni muuguzi mkunga katika hosptali ya wilaya ya mkuranga alisema changamoto nyingine ni kwa badhi ya watumishi wapya hawajui sheria na miongozo ya kazi hivyo kutoa ushauri kwa uongozi wa –TALGWU-kuweka mikutano ya Mara kwa Mara kwa wajumbe ili kuwasaidia kutambua haki zao katika utumishi.
TALGWU Mkoa wa Pwani wataendelea na ziara ya kukutana na wanachama wake katika wilaya ya CHALINZE,RUFIJI, BAGAMOYO na mkuranga na wataaendelea kutembelea wilaya zingine za mkoa huo ikiwa na lengo la kuzungumza na watumishi katika masula mbalimbali juu ya sheria za kazi,haki na wajibu ili kusaidia kupunguza migogoro ya mara kwa mara katika maeneo ya kazi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.