Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu Jenista Mhagama amewataka wawekezaji Nchini Kufuata kanuni taratibu na sheria wakati wanaendesha viwanda.
Akizungumza nao Viongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha nondo Fujin kilichopo kisemvule wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani leo Julai 6,2021 kiongozi huyo aliwahakikishia wawekezaji kuwa Rais Samia Suluhu Hassan hana nia ya kufunga viwanda vyenye kasoro bali anataka kazi iendelee wakati marekebisho yanaendelea kufanyika.
Waziri huyo amefurahishwa na baadhi ya marekebisho yaliyofanyika huku akimuagiza mwekezaji kutoa ushirikiano na taasisi husika kutatua changamoto ya mishahara,stahiki baada ya kuumia, na muda wa kazi.
Aidha kiongozi huyo aliahidi kuwaleta mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF) wakae Pamoja nao ili kuondoa sintofahamu kati ya mwajiri , wafanyakazi, na mfuko huo kuhusu usalama wa malipo yao.
Akiwa kiwanda kingine kinacho zalisha nondo na Plastiki cha Lodhia kilichopo kisemvule Waziri Mhagama alimpongeza Mkurugenzi wa kiwanda hicho ambaye ni Mtanzania Suleshi Pandit kwa uwekezaji wake mkubwa hapa nchini huku akimwahidi Serikali ya awamu ya sita itakua Pamoja nao kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili.
Awali Mkurugenzi Pandit alisema wanatengeneza nondo za mm (40) ambazo zinatumika kwenye ujenzi wa bwawa la Mwalimu Nyerere na daraja la Tanzanite sambamba na kuuza Nchi mbali mbali za Afrika huku wakijiandaa kuchakata makaa ya mawe yanayopatikana Mchuchuma.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Hadija Nasri alipongeza ujio wa Waziri huyo huku akimwahidi kufatilia kwa karibu utekelezaji wa maagizo yake kwenye ziara hiyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.