WAZAZI wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani wametakiwa kuwekeza kwenye elimu hasa ya watoto wa kike ili waweze kujikwamua kimaisha katika siku za usoni
Akizungumza na wazazi kwenye mahafari ya shule ya msingi Kisemvule iliyofanyika jana,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mkuranga Juma Abeid aliwataka wazazi na walezi waache tabia ya kutumia pesa nyingi kwenye sherehe za unyago, na ngoma za usiku badala yake watumie nguvu nyingi kuwekeza kwenye elimu ya watoto hao ili ije kuwasaidia kupata ajira na kujiajiri kutokana na uwepo wa viwanda wilayani humo
Aidha Juma Abeid ambaye pia ni Diwani wa kata ya Magawa aliwaagiza watendaji wa Vijiji, watumie vikao vyao kuhamasisha Wazazi, Wadau na Walezi wachangie pesa na vyakula kwa ajili ya watoto Mashuleni hali itayopaisha ufaulu na kupunguza utoro
Akizungumzia changamoto ya uzio wa shule alisema atatumia vikao vya Halmashauri kutenga Bajeti ya kwenye uzio. Awali Risala ya shule hiyo ilitaja changamoto ya utoro sugu kwa wanafunzi unaoathiri maendeleo ya kitaaluma shuleni na jamii kwa ujumla huku takwimu za mwaka huu zikiwataja wanafunzi (10) kutofanya mtihani wa Taifa kumaliza elimu ya msingi.
Aidha Wahitimu hao waliwaasa wanafunzi wenzao wanaobaki waendeleze nidhamu, utulivu na
usikivu muda wote watakao kuwa shuleni ili wawe mfano mzuri katika jamii na Taifa kwa
ujumla huku wakiwapa moyo wapambane hadi wazishinde changamoto.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.