Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani,inatarajia kufanya msako nyumba hadi nyumba ikiwa kwa lengo la kuwakamata wazazi ambao wamewaficha watoto wao wa kike ambao wamekatiza masomo kutokana na kupata ujauzito.
Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Wilaya hiyo,Mh Filbeto Sanga,katika kilele cha siku ya mtoto wa Afrika,kilichofanyika katika kijiji cha Magoza Kata ya Kiparang'anda. Sanga alisema kuna baadhi ya wazazi ambao wamewaficha majumbani watoto wao wa kike kutokana na kupata mimba na hali hiyo imesababisha kukatiza ndoto zao za kuendelea na masomo. "Kuna wazazi wanajua watoto wao ni wajawazito,wameacha shule wakakutana na familia iliyosababisha binti yao kupata ujauzito na kuzungumza na kumalizana,sasa Wilaya itafanya msako wa kimyakimya katika nyumba na mzazi akibainika kumalizana na aliyempa mimba binti yake anachukuliwa hatua," alisema.
Aliongeza kuwa Tanzania ya viwanda inahitaji wataalamu hivyo ni jukumu la wazazi kuhakikisha wanawapatia elimu watoto wao.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.