Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utawala bora na Utumishi wa umma Dkt. Mary Mwanjelwa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Eng. Mshamu Munde kuwasimamia maafisa ugani wa kata zote (25) ili wasaidie miradi ya kilimo na ufugaji kwa wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya masikini unaoendeshwa na TASAF.
Akiwahutubia wanufaika na wananchi wa kijiji cha Kiparang’anda baada ya kukagua bidhaa zao na kupokea ushuhuda kwenye uwanja wa ofisi ya kijiji, Dkt. Mwanjelwa ambaye pia ni Mbunge wa viti maalumu (CCM) mkoa wa Mbeya , alimpongeza Mratibu wa (TASAF) Wilayani humo ambaye pia Afisa maendeleo ya jamii; Safina Msemo kwa kuwapa shamba la ekari mbili sambamba na Tsh. Milioni 1 kikundi cha ‘Mwendokasi’ kilichopo Kise.
Akiendelea zaidi alimmwagia sifa mwalimu wa kujitolea, Mhandisi Komba ambaye anashirikiana nao katika mkakati wa kuwaendeleza na kujenga kiwanda cha chaki.
Aidha alizitaka Halmashauri zote nchini kuwatumia Maafisa Maendeleo ya jamii kwenye mipango ya TASAF.
Akitoa neno la shukrani Diwani wa kata ya Kiparang’anda , Miwadi Rashid; (ACT-Wazalendo) alimpongeza Waziri kuwa wa kwanza kuwatembelea pia amwambie Rais asiwaachanishe DC na DED
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.