Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali TAMISEMI Mhe Selemani Jafo amewaagiza viongozi wa Mkuranga kwenda kujifunza katika kituo cha afya Maneromango kilichopo wilayani Kisarawe ili waone jinsi matumizi ya force account yalivyoleta manufaa katika ujenzi wa vituo vya afya hapa nchini.
Jafo aliyasema hayo hapo jana wakati alipofanya ziara ya kutembelea kituo cha Afya Mkamba ili kujionea jitihada zinazoendelea baada ya Serikali kupeleka milioni 400 za ujenzi wa miundombinu itakayojengwa na fedha hizo zilizo tolewa na serikali na milioni 300 zingine zimepelekwa MSD kwa ajili ya ununuzi wa vifaa.
Aidha Jafo aliagiza ifikapo tarehe Aprili 30, mwaka huu majengo yote yawe yamekamilika.
Wakati huo huo Jafo alifanya ukaguzi wa barabara inayounganisha wilaya ya Mkuranga na wilaya ya Kisarawe kupitia bonde la Mkuruwili na amewaagiza meneja wa TARURA wa wilaya ya Mkuranga na wilaya ya Kisarawe kukaa pamoja kuiwekea mikakati barabara hiyo ili wananchi wa maeneo hayo waweze kuunganishwa vyema
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.