Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Angela Kairuki amewapongeza viongozi na wataalam wa Halmashauri ya wilaya ya mkuranga Mkoa Pwani kwa mikakati yao ya kuwavutia wawekezaji,
Akizungumza kwenye kijiji cha Mwanambaya baada ya kukagua ujenzi wa kiwanda cha “Fiber Solution” kiongozi huyo aliwahakikishia kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk John Pombe Magufuli itawashika mkono ili kufanikisha azma yao
Aidha Kairuki aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa kwa asilimia (100) na watanzania wazawa kufungua bohari Makao makuu ya serikali Dodoma sambamba na kusambaza mikoani
Awali mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho cha kutengeneza nyaya za mkongo Raddy Fiber Solution Ramadhani Hassan Mlanzi alisema pamoja na uzoefu na ukomavu katika teknolojia ya mawasiliano hasa mfumo wa Fiber wanakabiliwa na changamoto zikiwemo uagizaji wa bidhaa za waya na viunganishi toka nje ya nchi
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mhandisi Mshamu Munde alisema wamevutia wawekezaji kuja kuwekeza katika viwanda vya kilimo,uvuvi,na mifugo hadi kufikia June 2019 wana viwanda (71) vilivyoajiri watanzania 5424 kati ya hivyo viwanda vikubwa 12.
Munde alimhakikishia Waziri kairuki kuwa mkakati wao ni kufanya uwekezaji kuwa endelevu hatimaye kufanikisha kufikia uchumi wa kati kufikia (2025)
Akiwa wilayani mkuranga Kairuki alitembelea kiwanda cha marumaru MKIU kilichozinduliwa na Raisi Magufuli April 2017.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.