Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa Majaliwa ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Pwani kwa namna ilivyowezesha mazingira rafiki Kwa wawekezaji kupata maeneo ya kujenga viwanda sanjari na kutoa ajira kwa wakazi hao ili kujikwamua kiuchumi.
Waziri Majaliwa aliyasema hayo hapo jana wakati akifunga maonesha ya bidhaa za viwanda katika viwanja vya sabasaba Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani na kuelezea namna Serikali ilivyoboresha changamoto za kisera kwa kufanyiwa marekebisho ili kuhakikisha wawekezaji wanaongeza wigo mpana ili kukuza uchumi wa Viwanda.
Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage amesikitishwa na taasisi inayosimamia ubora wa bidhaa nchini TBS kutotekeleza majukumu yake kwa wakati na kusababisha moja ya Kampuni ya kuunganisha magari kuchelewesha kupata kibali.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng Evarist Ndikilo akitoa taarifa ya uwekezaji katika viwanda Mkoani humo alisema idadi ya viwanda vikubwa,vya kati na vidogo na jinsi mwamko wa wadau mbalimbali kujitokeza na kujenga viwanda.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh Selemani Jafo alisema katika ujenzi wa Hospitali zote za Wilaya wahakikishe wanatumia vifaa vinavyopatikana katika viwanda vya ndani.
Hata hivyo kabla ya kufunga maonyesho hayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitembelea ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa katika kijiji cha soga na kuridhishwa na hatua za ujenzi unavyoendelea.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.