Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa amezitaka Halmashauri zote Nchini kutumia Fedha za Mapato ya ndani katika kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo badala ya kusubili Fedha kutoa Serikali kuu pekee.
Ameyasema hayo leo tarehe 27/11/2022 alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba 6 vya Madarsa katika Shule ya Sekondari Mwandege iliyoko Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Aidha Mh. Waziri Majaliwa amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mwantum Mgonja kutenga kiasi cha Shilingi Milioni 120 kutoka katika Mapato ya Ndani ya Halmashauri hiyo, kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Utawala katika shule hiyo mara ifikapo mwezi Januari Mwakani.
Wakati huo huo Waziri Mkuu ametoa wito kwa Wakulima kuanza kulima kwani Mvua za kulimia ni hizi,
“viongozi wa dini mlituongoza kuomba dua Misikitini, Makanisani, tumeshuhudia mkiomba Mungu atushushie Mvua hii, basi si vibaya nikatoa wito kwa Wakulima kuwa mvua ya kwanza ndiyo Mvua za kupandia, twende tukaanze kazi ya kulima na kupanda mazao yenye uwezo wa kuota na kuiva kwa muda mfupi na tuweze kupata Chakula” Mh. Waziri alisisitiza
Pamoja na hayo Mh. Waziri Mkuu amemsimamisha kazi Mfamasia wa hospitali ya Wilaya ya Mkuranga Edwin Clement kwa kosa la kutotoa huduma ipasavyo kwa Mgonjwa Sharifa Saidi aliyekuwa alisumbuliwa na tatizo la Mkojo, amechukua uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na kitendo hicho.
“Mh Ulega umezungumza adha ya dawa, nimekasirishwa sana leo, dada yetu Sharifa binti Saidi kutoka Kisiju aliyekuwa anaumwa tatizo la Mkojo, alipokuja Hospitali alitakiwa afanyiwe Oparesheni akaagizwa vifaa kadhaa, ameenda kwa Mfamasia apate hivyo vifaa ili afanyiwe Oparesheni anaambiwa havipo wakati vipo ndani na anaambiwa aende akanunue dukani, huyu ni muuaji nimemsimamisha kazi” alisisitiza.
Waziri Mkuu yuko Ziarani Mkoani Pwani kwa muda wa siku tatu na bada ya kyfanya ziara Wilayani Mkuranga ataenda Wilaya ya Kibiti na atamalizia Ziara yake Wilaya ya Kisarawe tarehe 29/11/2022.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.