Waziri wa Habari Mawasiliano na Tekinolojia Dkt Ashatu Kijaji mwishoni mwa Juma alitembelea kiwanda cha Raddy Fiber kilichopo Kisemvule Wilayani Mkuranga ambacho kinatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni .
Dkt. Ashatu Kijaji amempongeza Mkurugenzi wa Raddy Fiber Bw.Ramadhani Mlanzi kuwa wapo Watanzania ambao wameweza kuwawezesha vijana wa kitanzani katika Ajira kwani wameonyesha mfano mkubwa sana katika viwanda vingine. Aidha Tanzania inalekea katika siku ya kusheherekea miaka 60 ya uhuru ya Tanzania hivyo kiwanda hiki ni moja ya mradi mkubwa unayotegemewa kuzinduliwa hivi karibuni
Mkuu wa Mkoa wa Pwani RC Mhe.Abubakar Kunenga Amempongeza Mkurugenzi pamoja na timu nzima ya kiwanda cha Raddy Fiber kwa kazi nzuri waliyofanya kwani kiwanda hicho ni cha nne kwa ukubwa katika Afrika na kimejipanga vizuri katika uzalishaji.
Aidha Naibu Waziri, Wizara ya mifugo na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mhe.Abdallah Hamis Ulega ameitaka serikali kuwaunga mkono wazalendo ambao wapo kwa ajili ya kuwekeza katika nchi yao na pia wajikite katika kuwakomboa vijana wa kitanzania kupitia ajira wanazowapa.Pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuwapatia fedha kwaajili ya ujenzi wa madarasa na kuhakikisha kuwa hakutakuwa na wanafunzi ambao wataingia kwa chaguo la pili .
Sambamba na hilo ameelezea changamoto ya mawasiliano katika wilaya ya mkuranga ambapo mtandao ni washida sana hivyo kupelekea shughuli nyingi kukwama.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Khadija Nassir Ali amemshukuru Waziri wa Habari ,Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari ,Dkt. Ashatu Kijaji kwa kuweza kutembelea kiwanda cha Raddy Fiber na kujionea jinsi walivyoweza kujiwekeza vizuri katika sekta ya viwanda kwa wawekezaji wa ndani na nje .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.