Mkuu wa Mkoa wa pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amewaonya wazazi wote wenye dhana potofu juu ya elimu bila malipo.Ndikilo aliyasema hayo wakati wa maadhimisho ya wiki ya elimu yaliyofanyika Kimkoa wilayani Mkuranga.
Mkuu wa Mkoa huyo alisema kwamba tafsiri potofu juu ya dhana ya elimu bila malipo ni miongni mwa mambo yanayorudisha nyuma ufanisi kiutendaji katika sekta ya elimu,hasa pale mzazi/mlezi anapoamini kwamba kila kitu kinafanywa na Serikali hata kama mambo mengine yapo ndani ya uwezo wa mzazi/mlezi hivyo tafsiri hii inaleta kikwazo kikubwa katika kutekeleza dhamira ya elimu bila malipo.
Waraka wa elimu Na.6 wa mwaka 2015 umezungumzia kuhusu utekelezaji wa elimu bila malipo ambapo umebainisha wazi majukumu ya kila mdau wa elimu kama Serikali,Wazazi/Walezi,walimu na Bodi za shule.
Jukumu mojawapo la wanajamii ni kuhamasisha wazazi au walezi kuandikisha watoto wote wenye umri lengwa,lakini pia kutoa ushirikiano kwa wazazi na walezi ili wanafunzi waweze kuhudhuria shule katika kipindi chote cha mafunzo.
Wiki ya elimu Mkoa wa pwani ulianza tangu tarehe tarehe 04 may 2017 kibaha na kuhitimishwa wilaya ya Mkuranga ambapo wilaya zote za mkoa wa pwani zilishirika kikamilifu kwenye sherehe hizo. Aidha sherehe hizo zilipambwa na maonyesho mbalimbali yaliyohusu elimu kuanzia ya awali mpaka vyuoni.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.