Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Filberto Sanga amekutana na viongozi wenza wa kamati ya Ulinzi na usalama Wilaya ya Kisarawe kwa lengo la kujadili njia stahiki zitakazotumika kutatua matatizo ya mipaka ya Ardhi ambayo imekua changamoto katika vijiji vinavyoungana kwenye Wilaya hizo.
Akizungumza na Maafisa Ardhi pamoja na viongozi wote wa kamati za ulinzi na usalama sanga ambaye pia anaongoza kamati ya ulinzi na usalama wilaya aliwaasa kuwa makini katika utatuzi wa changamoto hiyo na wajitahidi kufanya kazi hiyo kwa weledi na hatimaye kufikia malengo na kusudio la kikao hicho.
Aidha Afisa Ardhi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya kisarawe Jumanne Mwampashe alimuhakikishia sanga kufanya kazi kwa weledi na kusisistiza kuwa matokeo ya kazi hiyo yatakua chanya na hatimaye kuepuka vikao vya utatuzi wa ardhi kwa kila wakati
Sanga amewataka Mkuu Idara ya Kilimo,umwagiliaji na ushirika (DAICO) na Afisa Mifugo na maafisa wa vijiji kuanza kuwaondoa wafugaji wote ambao wamevamia maeneo ya mashamba ya watu na kurudishwa walikotoka na kaahidi kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Mkuranga itafika kuangalia utekelezaji huo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.