Takribani zahanati zaidi ya saba zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani zinatarajiwa kufunguliwa mapema mwaka huu, hii ni katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na mh Raisi Dk John Pombe Magufuli katika kuleta maboresho kwenye sekta ya afya..
Akizunguma katika Baraza la uwasilishwaji wa taarifa za kata za robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2019/2020 lililo fanyika katika ukumbi wa Flex Garden Diwani wa kata ya Tengelea na Mwenyekiti wa kamati ya uchumi na fedha Mh Shabani Manda amesema amefurahishwa sana na jinsi ambavyo Mkurugenzi mtendaji wa wilaya, sambamba na wakuu wa idara na vitengo wanavyosimamia vyema miradi inayoanzishwa na wanachi wa wilaya hiyo na hatimae kuiongezea nguvu na kuweza kufikia malengo ambayo mpaka sasa wanajivunia kupata zahanati saba ambazo wanatarajia kuzifungua na kuanza kufanya kazi mapema mwaka huu….
Aidha diwani wa kata ya Mkamba Mh. Hassani Dunda aliongeza kwa kusema anaridhishwa na maendeleo yanayoonekana katika Wilaya hiyo haswa upande wa elimu ambapo ndani ya kipindi cha miaka mitano wameweza kujenga sekondari tatu ikiwepo shule ya sekondari ya Abdalla Ulega iliyopo kata ya Tambani, shule ya sekondari mwandege iliyopo kata ya mwandege na shule ya sekondari miteza iliyopo kata ya njia nne……
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mkuranga na Diwani wa kata ya Magawa Mh. Juma Abeid aliongeza kwa kusema hana budi kumshukuru Mh Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaletea Mkurugenzi Hodari ambaye anajitoa kwa hali na mali na kutumia mda wa ziada katika kutekeleza na kusimamia majukumu yote yanayoihusu Halmashauri hiyo bila kujali mda anaotumia hata ule ambao anapaswa kupumzika
Diwani huyo wa Kata ya Magawa aliongeza kwa kusema kuwa anamuomba Mh Raisi Dkt. John Magufuli aendelee kumuacha Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya kwani ameonesha uadilifu na utiifu kwa kuzingatia ilani ya chama cha mapinduzi katika kusimamia miradi na kutimiza wajibu wake katika kazi..
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mhandisi Mshamu Munde aliwashukuru wakuu wa idara na vitengo kwa juhudi wanazozifanya za kusimamia miradi ya maendeleo na amewataka kusimamia ubora na viwango vya hali ya juu katika miradi yote inayoanzishwa ndani ya wilaya hiyo…..
Aidha mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga Ally Msikamo akitoa neno la shukrani amesema anawashukuru Madiwani wote, wakuu wa idara na vitengo kwa kujitoa kwa hali na mali na kuweza kusimamia ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kipindi chote walichokua madarakani pamoja na tofauti zilizokuwepo amekiri kuwa kuna wakati tofauti za mawazo na migongano huleta umoja na mshikamano katika kutafuta maendeleo ndani ya Wilaya….
Zahanati zinazotarajiwa kufunguliwa mwaka huu ni pamoja na zahanati ya Kuruti, Nganje, Tengelea, Mwarusembe, Kimanzichana, Nyatanga na Koma…
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.