Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh.Nicholas Kampa leo imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mradi wa daraja la Mvemle katika kijiji cha Hoyoyo kata ya Tengelea wilayani Mkuranga.
Daraja la Mvemle lilijengwa kutokana na changamoto ya kalavati dogo ambalo lilijengwa hapo awali lakini kutokana na mvua za Aprili-Mei kalavati lilisombwa na maji na hivyo kusababisha kutokuwepo kwa mawasiliano baina ya pande mbili za eneo hilo.
Aidha kutokana na udharula huo Halmashauri kupitia vikao vyake ikaamua kujenga daraja la dharula lililogharimu Tshs 25,770,000 ambapo fedha hizo zilitoka kwenye mfuko wa barabara (Road Fund).
Ujenzi wa daraja hilo ulitumia muda wa mwezi mmoja kuanzia tarehe 27/05/2017 na kumalizika 27/06/2017. Daraja hilo limekamilika kwa asilimia mia moja na linatumika kwa sasa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.