Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mh. Kambwili Shwahibu sambamba na timu ya Wataalamu chini ya Mhandisi Mshamu Munde imefanya ziara ya kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kwa lengo la kujifunza shughuli za ukusanyaji wa Mapato yatokanayo na mazao Bahari na Maswala mengine ya uvuvi.
Katika Ziara hiyo Waheshimiwa Madiwani na Wataalamu walipata fursa ya kuzitembelea (BMU) zilizopo Pangani Magharibi na Kipumbwi ambazo zimeonekana kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa Rasilimali za bahari pamoja na utunzaji wa mazingira ya Bahari na Pwani kwa ujumla.
Wakati wa Ziara timu ya wataalamu hawakusita kutoa pongezi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Ndg. Isaya Mbenje na Afisa Uvuvi wake kwa namna ambavyo wameweza kushirikiana na (BMU) timu ya ulinzi shirikishi ya rasilimali za uvuvi na kuweza kukusanya mapato mengi tofauti na matarajio ya kawaida
Aidha Madiwani na wataalamu waliahidi kutumia elimu waliyoipata katika kuamsha hali katika vijiji ambavyo vinafanya shughuli za uvuvi ambavyo tayari vilishakua na timu ya ulinzi shirikishi ya Rasilimali za uvuvi (BMU) ijapokua ilikosa usimamizi wa kina sasa wameahidi kwenda kuzisimamia vyema
“kwa kweli safari yetu kutoka jana mpaka leo imekua ya mafanikio tunashukuru sana, hiki ni kikao cha tatu lakini kila kikao kinakizidi kikao kingine tumefika Pangani Magharibi tukaona namna inavyofanya kazi na pia kusaidia jamii ila ajabu tumefika hapa kipumbwe ndo tumechoka kabisa kumbe tungesema tuishie kule tungekosa mambo ya maana sana. Tukasema au kwa sababu mwenyekiti wa Halmashauri na Diwani wa Kipumbwe anatoka hapa ndo mana Kipumbwe mambo mazuri lakini si dhambi ukiwa sehemu uliyopo ukatengeneza mambo mazuri Zaidi kwa lengo la kusaidia jamii unayoiongoza lakini pia kuacha alama hata baada ya kumaliza uongozi wako”
Naye Mhandisi Munde aliongeza kwa kusema tunakazi kubwa ya kufanya sio tu katika kuunda na kuhamasisha watu kujihusisha na shughuli za BMU lakini pia kuwapa hamasa wananchi kujihusisha na shughuli zenyewe za uvuvi ili mwisho wa siku hata wanaposhughulikia mapato na kuunda BMU iwe na maana na ilete tija kwa wananchi wa maeneo yaliyozungukwa na bahari.
Munde aliendelea kwa kusema wananchi waliowakuta pale wameonesha kutokua na hofu wala mashaka na Serikali yao na wameonesha kuwa tayari kulipa kodi bila ya ushawishi mkubwa kwa namna ambavyo wameshiba elimu waliyopewa na viongozi wa Kijiji na Wilaya kwa jinsi wanavyowajibika katika ukusanyaji wa mapato na pia kusimamia vyema asilimia wanayorejeshewa kwa kuitumia katika kuleta maendeleo katika vijiji vyao na kwenda mbali kwa kusaidia kaya zenye uhitaji kwa kuwanunulia Watoto mavazi ya shule na madaftari sambamba na kutumia fedha hizo katika kuboresha miundo mbinu ya Elimu..
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.