Kamati ya Elimu, Afya na Maji ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh Shaban Manda na wataalam mbalimbali jana walitembelea miradi ya maendeleo ikiwemo jengo la zahanati kuruti.zahanati hiyo imejengwa kwa nguvu za wananchi na Halmashauri imechangia mil 25 na hatua iliyofikia mpaka sasa bado umaliziaji wa jengo hilo yaani" Finishing"
Aidha Mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Rajabu Shaban amemuomba Mbunge wa Mkuranga Mh Hamis Abdallah Ulega kupitia mfuko wake wa jimbo kuweza kusaidia umaliziaji wa zahanati hiyo ili kurahisisha huduma ya afya na kupunguza vifo vitokanavyo na wakina mama na watoto.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ameahidi kuongea na Ulega ili kutatua changamoto ya zahanati hiyo,lakini pia kulisemea kwenye vikao mbalimbali ili kunusuru afya za wakazi wa kijiji hicho.
Pia kamati ilitembelea shule ya sekondari Shungubweni ambapo iliona mradi wa maabara ambapo jengo la mradi huo umekamilika kwa asilimia 80 isipokua bado umaliziaji wa plasta,gypsum na kuweka milango na fenicha.
Mkuu wa Shule hiyo mwalimu Selemani Yusufu alisema vifaa vyote ya maabara serikali iliwaletea na vipo vya kutosha na wanasubiri vyumba vya maabara vikamilike ndipo vikae mahali husika kwa ajili ya matumizi ya masomo ya sayansi.
Mkuu huyo ameiomba kamati hiyo kufanya umaliziaji wa maabara hiyo ili kuleta tija katika kufudisha masomo ya sayansi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.