Leo tarehe 17/08/2022 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Hadija Nasri Ali amepokea ugeni kutoka Tume ya Madini ikiongozwa na Mwenyekiti wake Prof.Idris S.Kikula na wataalam mbalimbali waliofika kwa lengo la kutembelea miradi mbalimbali ya Madini Wilaya hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Hadija Nasri Ali akiongozana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bi.Mwantum Mgonja na Katibu Tawala Bi.Veronica Kinyemi pamoja na wataalam wa Wilaya wametembelea miradi mikubwa miwili ambayo ni NEEL KANTH GROUP na FOREVER REACH MINING ambayo ipo katika Kata ya Shungumbweni na kukagua maendeleo ya uzalishaji,mazingira ya wafanyakazi na kufatilia ulipaji kodi wao kwa serikali na wavyosaidiana na jamii.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.