Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhandisi MshamuMunde jana amefungua mafunzo maalumu kwa wawezeshaji watakaoenda kufanikisha zoezi la uhakiki kwa walengwa wanaofaidika na mradi wa kusaidia kaya masikini (TASAF) unaotarajiwa kuanza mapema mwishoni mwa wiki hii..
Katika hotuba yake Mhandisi Munde alisisitiza kuwa mafunzo haya yanatolewa kwa lengo la kuwapa uelewa na utaratibu wa namna gani uhakiki utafanyika ukizingatia uhakiki wa mwaka huu unafanywa kwa njia tofauti na vitatumika visukwambi kwa ajii ya uhakiki huo.
Munde alisisitiza kuwa hili zoezi ni la muhimu kwa sababu lengo kubwa ni kuondoa kaya hewa kama zipo ili kuwa na idadi ya watu kamili ambao wanastahili kupata msaada huu
“Katika mazoezi kama haya mara nyingi tunapenda sana uadilifu wa watendaji ambao wametumwa kufanya hiyo kazi na ndio maana kipindi hiki wakati wa kufanya mafunzo haya tunataka wawezeshaji ambao wataenda kufanya zoezi la uhakiki waape na maana ya kiapo ni kwamba wakishafanya kazi na ikagundulika kuwa ni kazi mbaya watawajibishwa kulingana na kiapo chao” alisisitiza
Naye Mkurugenzi wa TASAF ndugu Adslaus Mwamanga ambaye amewakilishwa na bi Mary Mtambalike alisema tathmini ya utekelezaji wa kipindi cha kwanza cha awamu ya tatu ya TASAF inaonyesha kuwa mpango wa kunusuru kaya Maskini umechangia kwa kiasi kufikiwa azma ya serikali ya kupunguza umaskini nchini.
Sambamba na hili Mwamanga alisisitiza Takwimu zinaonyesha kwamba utekeleza wa mpango kwenye kipindi cha kwanza umechangia kupungua kwa umaskini wa mahitaji ya msingi kwa kaya kwa asiimia 10 na umasikini uliokithiri umepungua kwa asilimia 12 kwa kaya maskini nchini.
Zoezi hili la uhakiki linafanyika kutekeleza agizo la Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli wakati alipotoa agizo februari mwaka huu kwamba kabla ya shughuli zozote za kipindi cha pili kuanza, uhakiki wa walengwa ufanyike kote nchini ili kuondoa kaya zote za walengwa ambazo zimepoteza sifa .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.