MKUU wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nasri ametoa wito kwa wataalamu na wasimamizi wa zoezi la anuani za makazi kuhakikisha wanawabainisha wananchi ambao hawapo kwenye maeneo yao ili zoezi hilo lisije likahalalisha uharamu wa wananchi wanaoishi kwenye maeneo kinyume na taratibu.
Khadija ametoa wito huo wakati akizindua zoezi la anuani za makazi katika Wilaya hiyo lililofanyika kwenye mtaa wa boma ilipo ofisi ya Mkuu wa wilaya.
Amesema Wataalamu na wasimamizi wa anuani za makazi wanatakiwa kuendelea kubainisha wananchi ambao hawapo kwenye maeneo yao rasmi kwani wakirasimishwa kwenye zoezi hilo ina maanisha tayari tayari wamehalalishiwa makazi yao maeneo ambayo sio rasmi kwao.
Aidha ametoa agizo kwa wataalamu kutumia vizuri fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kazi hiyo iweze kuka kwa wakati ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano kwa vijana wanaofanya kazi hiyo katika maeneo ya kata na vijiji.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Jessy Mpangala amesema tatizo la kutokujua umuhimu na faida ni chanzo cha vikwazo kwenye zoezi hilo.
Jessy amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo kutoa elimu kwa wananchi pindi wanapoenda kutekeleza majukumu yao ili kuondoa ugumu wa anuani za makazi.
"Ipo faida ya anuani za makazi ambapo biashara zinaweza kufanyika kwa urahisi kwa njia ya mtandao lakini pia inaimarisha ulinzi na usalama pamoja na ajira" ameeleza.
Mratibu wa anuani za Makazi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Denis Myovela amesema gharama za zoezi hilo nia sh. Miln 178,840.
Aidha amebainiha kuwa kati ya fedha hizo tayari wamepokea sh. Miln 81,629,248 kutoka serikali kuu na kwamba kiasi kilichobaki sh. Miln 97,210,751.91 zitatoka kwenye mapato ya ndani.
Hamashauri hiyo imejipanga kumaliza zoezi la anuani za makazi mwishoni mwa mwezi April na kujipamuda wa kufanya marekebisho kabla ya sensa ya makazi mwezi Agost.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.