Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mkuranga, Mkoa wa Pwani Mhandisi Msham Munde, ametangaza rasmi kuwa kituo cha utoaji wa fomu za wagombea wa Ubunge na Udiwani walioteuliwa na vyama vyao vya siasa ofisi ziko wazi kuanzia leo tarehe 12/8/2020 mpaka siku ya tarehe 25/8/2020
Aidha vituo vyote vitakua wazi kuanzia saa moja na nusu asubuhi na kufungwa saa kumi kamili jioni, zoezi hili litahusisha uchukuaji wa fomu za uteuzi wa wagombea ubunge kwa ngazi jimbo na fomu za uteuzi kwa madiwani amabazo zitatolewa katika ofisi za wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata.
Sambamba na hilo msimamizi wa uchaguzi amewahakikishia wagombea wote wenye nia ya kuchukua fomu za uteuzi kwa nafasi za Ubunge na Udiwani kuwa wasimamizi wa uchagui watakuwa kwenye ofisi za utoaji wa fomu mda wote ulioainishwa kisheria
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.