TAARIFA YA WILAYA YA MKURANGA YA HALI YA HUDUMA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA VIJIJINI:
Utangulizi:
Wilaya ya Mkuranga ina hali ya hewa ya joto la wastani wa nyuzi joto 28.Wilaya inapata misimu miwili ya mvua yaani masika na vuli. Wastani wa mvua hizi ni milimita 800 hadi 1000 kwa mwaka. Mvua za masika kawaida hunyesha kati ya miezi ya Machi hadi Juni, na mvua za vuli hunyesha kati ya miezi ya Oktoba hadi Desemba. Katika miaka ya hivi karibuni mvua hizo zimekuwa ni haba kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Hali hii imechangia sana kukauka kwa vyanzo vya maji, hususan katika maeneo yenye huduma ya maji ya visima vifupi.
Vyanzo vikuu vya maji katika wilaya ya Mkuranga, ni pamoja na uvunaji wa maji ya mvua, maji ya chini ya ardhi (Underground Water), Chemichemi na Mabwawa. Mpaka Juni, 2017 jumla ya wakazi 123,623 wanapata huduma ya majisafi na salama.. Hii ni sawa na asilimia 62.5 ya wakazi wote 197,797 wa Mkuranga waishio vijijini. Vilevile asilimia kumi (10) ya wakazi wa Mji wa Mkuranga ndio wanaopata huduma ya maji safi na Salama
Huduma ya Maji:
Mpaka kufikia tarehe 30 Juni 2017, huduma ya maji katika wilaya ya Mkuranga maeneo ya vijijini yamekuwa yakipata maji kwa wastani wa asilimia 62.5. Aidha, huduma hii hutolewa kwa kutumia miundombinu ya maji ya mitandao ya bomba, visima virefu na vifupi vya pampu za mkono na zinazoendeshwa na mitambo ya Genereta za nishati ya mafuta, umeme wa nguvu ya Jua na mifumo ya kuvuna maji ya mvua.
Aidha, jumla ya wakazi 2512 wa makao makuu ya Halmashauri ya Mkuranga, wamekuwa wakipata maji safi na salama sawa na asilimia 10 ya wakazi wote wa mji. Mji huu hupata maji kutoka katika chanzo ambacho ni kisima kirefu kilichopo eneo la Kulungu.
Jedwali namba 1 na 2 hapa chini yanaonyesha viwango vya upatikanaji wa huduma ya maji katika Vijiji na mji wa Mkuranga.
Jedwali Na 1: Viwango vya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa vijijini katika wilaya ya Mkuranga kufikia tarehe 30 Juni 2017
Na
|
Halmashauri
|
Idadi ya watu (sensa) 2012
|
Kiwango cha upatikanaji wa maji (%)
|
|
Waliopo
|
Wanaopata maji
|
|||
1
|
Mkuranga
|
197,797 |
123,623 |
62.5 |
Jedwali Na 2: Viwango vya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa Mjini Mkuranga (makao makuu ya Halmashauri ) ya wilaya ya Mkuranga kufikia tarehe 30 Juni 2017.
Na
|
Halmashauri
|
Idadi ya watu (sensa) 2012 |
Kiwango cha upatikanaji wa maji (%) |
|
Waliopo
|
Wanaopata maji
|
|||
1
|
Mkuranga
|
25,124 |
2510 |
10 |
UTEKELEZAJI WA MIRADI KATIKA VIJIJI 10 KATIKA HALMASHAURI
Mkuranga ni wilaya mojawapo katika Mkoa wa Pwani inayotekeleza miradi ya maji vijijini chini ya Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP). Katika hatua za awali za utekelezaji wa programu hii, kumekuwa na utekelezaji wa miradi midogo inayoleta matokeo ya haraka. Miradi hii ilitekelezwa katika miaka ya 2007/2008 na 2008/2009. Fedha za kutekeleza miradi hiyo zilisitishwa kutolewa mwezi Juni 2009 ili kuanza kutekeleza miradi mikubwa ya vijiji 10 katika kila Halmashauri kupitia WSDP katika mpango wa Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP). Vijiji vilivyopewa kipaumbele ni kama ilivyoonyeshwa kwenye Jedwali Na 3 hapo chini.
Jedwali Na. 3: Vijiji Vilivyopewa Kipaumbele na Halmashauri katika kutekeleza Programu - Awamu ya Kwanza.
HALMASHAURI |
VIJIJI |
Mkuranga
|
Kilamba, Mvuleni, Kilimahewa kusini, Mandimkongo, Mandimpera, Tundu, Tipo, Bupu, na Nyanduturu
|
Jedwali Na 4: Hatua ya utekelezaji wa miradi ya maji vijijini kwa mpango wa vijiji 10 katika Halmashauri kupitia WSDP hadi 30 June 2017
Halmashauri
|
Jina la mradi
|
Vijiji husika
|
Asilimia ya utekelezaji
|
Maoni
|
Mkuranga
|
Mradi wa maji ya bomba wa Kilamba
|
Kilamba
|
100 |
Mradi umekamilika.
|
Mradi wa maji ya bomba wa Mvuleni/Kilimahewa kusini
|
Mvuleni na Kilimahewa kusini
|
100 |
Mradi umekamilika.
|
|
Mradi wa maji wa visima 9 vya pampu za mkono.
|
Mandimkongo,Tundu Mamdimpera, na Kilimahewa kusini
|
100 |
Mradi umekamilika.
|
|
Mradi wa maji ya bomba wa Bupu.
|
Bupu
|
100 |
Mradi umekamilika.
|
|
Mradi wa maji ya bomba wa Nyanduturu.
|
Nyanduturu
|
100 |
Mradi umekamilika.
|
|
Mradi wa maji ya bomba wa Tipo.
|
Tipo
|
100 |
Mradi umekamilika.
|
Maandalizi ya utekelezaji wa programu ya maendeleo ya sekta ya maji (WSDP) awamu ya pili
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imeainisha vijiji 8 vitakavyotekelezwa miradi katika awamu ya pili ya program (WSDP II).
Utekelezaji: Kufikia Juni 2018 Wilaya ya Mkuranga inatarajia kutekeleza miradi katika jumla ya vijiji 8 ambavyo vitapatiwa Maji safi na Salama kupitia program ya maendeleo ya sekta ya maji awamu ya pili (WSDP II), Vijiji hivyo ni Mkerezange, Kimanzichana, Ng’ole, Mdimni, Mwanambaya, Yavayava, Mlamleni na Mbulani mpaka sasa tayari shughuli ya uchimbaji wa visima katika vijiji hivyo umekamilika kwa asilimia 100, kazi iliyopo mbele yetu tunatengemea kuanza kufanya Usanifu wa miradi mapema pindi tu tutakapopokea fedha kwa ajili ya Usanifu wa Miradi hiyo.
Lengo ni kuongeza huduma ya maji kutoka asilimia 62.5 mwaka 2017 hadi asilimia 70.5 ifikapo mwezi Juni 2018 .
JEDWALI No 5 LA MIRADI MIPYA INAYOTARAJIWA KUTEKELEZWA 2017-2018
Jina la kijiji
|
Jina la mradi
|
Kazi iliyofanyika
|
Kazi inayotarajiwa kuanza
|
Idadi ya watu wakaopata huduma ya maji baada ya kukamilika kwa mradi
|
Idadi ya vituo vitavyojengwa
|
Kimanzichana
|
Kimanzichana
|
Uchimbaji umekamilika
|
Usanifu wa Mradi
|
15,456 |
|
Mkerezange
|
Mkerezange
|
Uchimbaji umekamilika
|
Usanifu wa Mradi
|
1,397 |
|
Ng'ore
|
Ng'ore
|
Uchimbaji umekamilika
|
Usanifu wa Mradi
|
1,021 |
|
Mdimni
|
Mdimni
|
Uchimbaji umekamilika
|
Usanifu wa Mradi
|
1,032 |
|
Mwanambaya
|
Mwanambaya
|
Uchimbaji umekamilika
|
Usanifu wa Mradi
|
4,823 |
|
Yavayava
|
Yavayava
|
Uchimbaji umekamilika
|
Usanifu wa Mradi
|
993 |
|
Mlamleni
|
Mlamleni
|
Uchimbaji umekamilika
|
Usanifu wa Mradi
|
7,886 |
|
Mbulani
|
Mbulani
|
Uchimbaji umekamilika
|
Usanifu wa Mradi
|
2,561 |
|
JUMLA |
35,169 |
70 |
UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI KUPITIA MAPATO YA NDANI ( OWN-SOURCE) NA RUZUKU KUTOKA SERIKALI KUU (LGCDG) .
Katika kutekeleza Miradi ya maji vijijini Wilaya ya Mkuranga imekuwa ikitenga fedha kupitia mapato ya ndani na fedha za ruzuku kutoka serikali kuu ili kuwezesha huduma ya upatikaji wa Maji safi na salama kwa wananchi.
Hadi kufikia Juni 2017 Jumla ya Miradi 4 imekekelezwa kupitia mipango hiyo
Jedwali No 6
Jina la kijiji
|
Jina la mradi
|
Kazi iliyofanyika
|
Hatua iliyofikiwa
|
Mkerezange
|
Mkerezange
|
Ujenzi wa Mradi mdogo wa Maji (unatumia Generator)
|
100 |
Panzuo
|
Panzuo sekondary
|
Ujenzi wa Mradi mdogo wa Maji (unatumia nguvu ya jua)
|
100 |
Mkuranga
|
Mradi wa Maji Sokoni
|
Ujenzi wa Mradi mdogo wa Maji (unatumia Generator)
|
100 |
Mkwalia Kitumbo
|
Kulungu
|
Uchimbaji wa kisima
|
100 |
Nasibugani
|
Nasibugani Sekondari
|
Ujenzi wa Mradi mdogo wa Maji (unatumia Generator)
|
100 |
UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI KUPITIA WADAU WENGINE WA MAENDELEO .
Katika Wilaya Mkuranga wapo wadau mbalimbali walioshirikiana na serikali katika kuwapatia maji wakazi wa wilaya hii ambao ni pamoja na:
Shirika la ushirikiano wa kimataifa la Japan (JICA) ambalo limejenga miradi ya maji ya bomba katika vijiji vya Mwandege/Kipala, Vianzi, Mfurumwambao/Marogoro, Kisemvule na Njopeka inayotumia umeme wa jenereta.
Aidha shirika la AFRICAN REFLECTIONS wamejenga miradi midogo midogo ya maji ya bomba katika maeneo yafuatayo ambayo ni:
Kiparang'anda, Kisima Sekondari, Nyatanga, Dundani Shule ya Msingi, Ngunguti Shule ya Msingi, Kiguza Shule ya Msingi, Vianzi Shule ya Msingi, Misasa Shule ya Msingi, Zahanati ya Lukanga na Zahanati ya Mbezi Msufini.
miradi hii hutunmia umeme wa nguvu za jua,
HUC ( HELPED UNDESERVED COMMUNITIES) Shirika hili limeweza kushirikiana na Halmshauri kwa kuchimba visima vifupi zaidi ya 40 katika Kata ya Mkuranga, Nyamato, Bupu, Dundani, Kisiju, Panzuo, Kimanzichana Tambani, Kitomondo, Njianne Mbezi na Shungubweni na kufunga Pampu za mikono.
BALOZI WA KUWEIT:
Balozi wa Kuweit kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Tanzania ameweza kuchimba visima sita (6) ambavyo ni Zahanati ya Kalole, Vijiji vya Msonga, Kisayani, Shungubweni na Kerekese Shule ya Msingi.
UUNDAJI NA USAJILI WA JUMUIYA ZA WATUMIA MAJI KATIKA WILAYA YA MKURANGA
Kuunda na kusajili vyombo vya uendeshaji (COWSOs) na usimamizi wa miradi ya maji 8 ifikapo mwezi Juni mwaka 2018.
Utekelezaji: Uundaji na usajili wa jumuia za watumiaji maji umepangwa kufanyika mwaka 2017/2018 na kuendelea. Hata hivyo, kufikia mwezi Juni 2017 jumla ya Vyombo huru 22 vya watumiaji maji viliundwa na 14 kusajiliwa.
HALI YA UPATIKANAJI WA FEDHA.
Katika kipindi cha mwaka 2016/2017 Halmashauri ilitengewa kiasi 1,187,360,000 cha fedha kilichopelekwa kwenye Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga ni shilingi 102,230,000 Kiasi cha fedha zinazotengwa kwa ajili ya halmashauri kinazingatia kiwango kilichopo cha huduma ya maji, wingi wa watu, aina ya teknolojia inayotumika na kufuzu au kutofuzu vigezo vya kupata ruzuku ya maendeleo kutoka serikalini kwa kila Halmashauri. Fedha zilizotengwa kwa ya utekelezaji wa vijiji 8 kwa mwaka 2017/2018 ni kama inavyoonyeshwa kwenye Jedwali No 9 hapo chini.
Fedha Zilizotengwa na zilizopokelewa kwa Mwaka 2016/2017 kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi Jedwali No. 8
Halmashauri
|
Aina
|
Fedha zilizotengwa
|
Fedha zilizopokelewa
|
Asilimia
|
Mkuranga |
DC |
1,187,360,000 |
102,230,000 |
8.6 |
Jedwali No. 9: Fedha Zilizotengwa kwa Mwaka 2017/2018 kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi ya Vijiji 8
Jedwali No. 9
Halmashauri
|
Aina
|
Fedha zilizotengwa
|
Fedha zilizopokelewa
|
Asilimia
|
Mkuranga
|
DC |
803,656,000 |
- |
0 |
CHANGAMOTO
Pamoja na mafanikio yote yaliyopatikana katika kutekeleza miradi, kuna changamoto zililzojitokeza kama ifuatavyo:-
Upungufu wa watumishi katika idara ya maji
Uchakavu wa miundombinu ya maji hasa mjini Mkuranga
Kutopatikana fedha kwa ajili ya mradi wa maji mjini Mkuranga ili kupanua huduma
Kuchelewa kupata fedha za kulipa wakandarasi pindi wanapomaliza kazi
Baadhi ya vyombo vya watumia maji kutomudu vema majukumu yao ya kusimamia miradi
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.