Kuongezeka kwa viwanda kutoka viwanda 45 mwaka 2015 , hadi viwanda 57 vilivyopo sasa..Kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wafanyabiashara wapatao 901
Kushikiana na sekta binafsi kutenga maeneo mahususi kwa uwekezaji wa viwanda katika maeneo ya Mkiu(ekari 1000),Kisemvule (ekari 9), na kubainisha kwa kuwashiikisha wananchi kutenga maeneo ya Dundani(ekari 700) na Mbezi(ekari 10,000)
Kuna jumla ya Viwanda 57 ambavyo vimegawanyika kama ifuatavyo
Viwanda vikubwa 06
Viwanda vya kati 13
Viwanda vidogo 38
Viwanda vimewezesha watanzania 7110 kupata ajira za kudumu na muda mfupi ambapo wanaume 4977 na wanawake.
Mafanikio yaliyopatikana ni kuongezeka kwa kipato kutokana na ushuru wa huduma na leseni za biashara kwa viwanda vidogo.
Mji wa Mkuranga pia unazidi kukua zaidi kutokana na ongezeko la idadi ya watu.
Mikakati iliyopo katika kuvutia wawekezaji ni kwamba ulinzi na usalama wa raia na wageni umeimarishwa, pia maeneo maeneo kwa ajili ya wawekezaji kama dundani na mbezi.Pia kuwashirikisha wananchi juu juu ya ujio wa wawekezaji na aina ya mradi anaotaka kuwekeza na faida watakazopata jamii inayozunguka mradi huo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.