TUKASIMAMIE ILANI YA UCHAGUZI
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mohamed Dau amewataka Madiwani wa halmashauri hiyo kuisimamia vema Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.
Mhe. Dau ameyasema hayo Desemba 3, 2025 kwenye ukumbi wa Halmashauri na kusisitiza kuwa kufanya hivyo ni dalili tosha ya kumuunga mkono Mh. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassani ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mkuranga Juma Magahila amewaomba Madiwani hao kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kuifanya Mkuranga iendelee kuwa sehemu bora na salama kwa wageni wanaotaka kuja kuwekeza.
Akitoa Salam za Serikali Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ali ametoa rai ya kufanyika kwa semina elekezi kwa Madiwani hao kwa haraka ili kila mmoja ajue majukumu yake na kumuwezesha kufanya kazi na kutekeleza malukumu yao kwa weledi.
Amesema pamoja na kupata semina hiyo anaamini Madiwani hao watakuwa Madaraja ya kuwafikia wananchi na kuweza kuwasikiliza vema na kutatua kero na changamoto za wananchi ili waendelee kuiamini Serikali yao.
"Tunatakiwa kuwa wamoja ili kuweza kuwatumikia wananchi wa Mkuranga na tuweze kushirikiana kuweka mbele maslahi mapana ya wananchi, alisema Mkuu wa Wilaya"
Aidha amesisitiza kuwa uchaguzi umekwisha hivyo zile ahadi zikizokuwa zikinadiwa majukwaani ziende zikafanyiwe kazi ndani ya vikao vya Baraza ili kuweza kufanyiwa kazi na kuleta tija kwa wananchi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.