Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ali tarehe 26, Novemba amefanya ziara ya kukagua miradi miwili mmoja ukiwa ni wa ujenzi wa jengo jipya ya ukumbi wa kisasa pamoja na mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya Mwandege
Mradi wa kwanza kuutembelea ulikuwa ni wa ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa Mikutano ambao mpaka sasa umetengewa kiasi cha shilingi Bilioni 1.63 ambao unatekelezwa katika Kijiji cha Mkwalia Kata ya Mkuranga.
kwa fedha za mapato ya ndani kwa utaratibu wa Kandarasi
Aidha mradi huo wa ukumbi wakisasa utakuwa na uwezo wa kuchukua watu wasiopungua 600 kwa wakati mmoja na ukumbi mdogo utakaoweza kuchukua watu 40 sambamba na hilo utakuwa na vifaa maalum vya Teknolojia na mawasiliano kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano wakati wa Mikutano au vikao.
Mradi mwingine aliokagua ni ule wa ujenzi wa kituo kipya cha Afya kinachojengwa Kijiji cha kipala Mpakani ambacho kimetengewa kiasi cha shilingi Milioni 200.5 ikiwa zimepokelewa kutoka Serikali kuu.
Fedha hizo zimepangwa kutekeleza ujenzi wa jengo la OPD, matundu matano ya vyoo na kichomea Taka cha kisasa ambapo ujenzi huo unatarajia kukamilika mwezi wa 12 Mwaka huu.
Awali akiwa katika eneo la ujenzi wa Kituo hiko cha Afya Mkuu wa Wilaya amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Waziri kombo pamoja na wataalamu wa Afya kujipanga mapema kwani Kituo hiko kikikamilika kuna uwezekano mkubwa kuhudumia na wananchi kutoka Dar es Salaam
Sambamba na hilo ameelekeza kulinda mipaka ya eneo hilo kwa kulitafutia hati pamoja na kuwa na mpango mzuri wa matumizi sahihi ya ardhi utakaowezesha kupanga majengo mengine mara fedha nyingine zitakapokuja.
Ziara hii ni mwendelezo wa ziara za Mkuu wa Wilaya kukagua na kuona utekelezaji wa miradi ya maendeleo Wilayani Mkuranga ikiwa ni ndani ya siku 100 za Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.