MAJUKUMU YA IDARA YA ELIMU MSINGI
Kufafanua na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo. Sheria na kanuni zinazoongoza utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi.
Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu masuala yote ya kielimu katika Halmashauri.
Kusimamia shughuli za Taaluma katika Wilaya.
Kusimamia na kuratibu mitihani ya Darasa la II, IV, VII na MOCK ya Elimu ya Msingi.
Kusajili wanafunzi waliopo mfumo rasmi / nje ya mfumo rasmi.
Kusimamia na kuratibu mpango wa walimu kujiendeleza.
Kushughulikia upanuzi wa Elimu katika ngazi ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi.
Kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya elimu kila mwaka.
Kudhibiti matumizi ya fedha za elimu kwa mujibu ya miongozo ya fedha za serikali.
Kuthibitisha kwamba shule zote zinainua ubora wa mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Kusimamia wajibu na haki za walimu.
Kukusanya, kuratibu na kuchambua takwimu za elimu katika Halmashauri kwa ajili ya mipango ya maendeleo katika ngazi ya shule, Halmashauri , Mkoa na Taifa.
Kusimamia, kuratibu na kutathimini mipango mbalimbali ya EWW na MEMKWA na MUKEJA.
Kuratibu utoaji wa Elimu masafa, ya ana kwa ana, kwa kushirikiana na mkufunzi wa makazi wa elimu ya watu wazima Mkoa na Waratibu wa vituo katika Sekondari na vyuo (learning centres).
Kusimamia uandaaji wa taarifa za TWM za kila robo mwaka na uagizaji wa vifaa vya EWW.
Kufanya makisio ya idadi ya mahitaji ya walimu.
Kufuatilia huduma kwa wanafunzi K.M. Mahudhurio, Uhamisho na chakula cha mchana.
Kusimamia miradi ya maendeleo hususani miundombinu shuleni.
Kufuatilia utelekelezaji wa taarifa za Ukaguzi wa shule za msingi.
Kusimamia maendeleo ya Taaluma na michezo (UMITASHUMTA)
Kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu maalumu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Kubuni mbinu mbalimbali za kuinua taaluma.
Kusimamia na kuratibu shughuli za sayansi kimu shuleni.
Kufanya ziara za ufuatiliaji wa Taaluma na miundombinu.
Kufanya kazi nyingine kama itakavyoelekezwa na Mkurugezi Mtendaji Wilaya wa Halmashauri.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.