TAARIFA FUPI YA WILAYA (DISTRICT PROFILE)
1.1 MAHALI ILIPO
Wilaya ya Mkuranga ni mojawapo kati ya Wilaya 9 za Mkoa wa Pwani. Ipo katikati ya latitude 6o.35 o na 7o.15o Kusini mwa Ikweta; na Longitudi 38o.15o na 39o.30o Mashariki mwa Meridian. Wilaya ya Mkuranga inapakana na Wilaya ya Temeke kwa upande wa Kaskazini, Ilala upande wa Kaskazini Magharibi kwa upande wa Kusini inapakana na WIlaya ya Wilaya ya Kibiti, Upande wa Mashariki inapakana na Bahari ya Hindi na upande wa Magharibi inapakana na Wilaya ya Kisarawe. Wilaya ya Mkuranga ina ukubwa wa eneo la Km. za mraba 2,432 kati ya hizo Km. za mraba 447 ni za maji (Bahari ya Hindi) na Km. za mraba 1985 za nchi kavu ambapo eneo la km. za mraba 1934 linafaa kwa kilimo.
HALI YA HEWA NA SURA YA NCHI
Wilaya ya Mkuranga ipo katika ukanda wa mashariki mwa Pwani ya Bahari ya Hindi. Hali ya hewa ni ya kuridhisha, Wilaya hupata mvua katika vipindi 2 kwa mwaka. Kipindi cha Novemba hadi Desemba (Vuli) na kipindi cha mwezi Machi hadi Juni (Mvua za Masika). Kwa wastani Wilaya hupata mvua kati ya mm.800 hadi mm.1,000 kwa mwaka na wastani wa nyuzijoto 28o.
IDADI YA WATU
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya Taifa ya mwaka 2012, wakazi wa Wilaya ya Mkuranga ni 222,921 wakiwemo wanawake 108,024 na wanaume 114,897. Ikiwa na ongezeko la watu la wastani wa asilimia 2.0 kwa mwaka.
UTAWALA
Wilaya imegawanyika katika Tarafa 4, Kata 25, Vijiji vilivyosajiliwa 125 na Vitongoji 477. Mchanganua wa kiutawala na idadi ya watumishi imeoneshwa katika jedwali 1 na 2
Jedwali 1. Mgawanyo wa Kiutawala
MWAKA |
TARAFA |
KATA |
VIJIJI |
VITONGOJI |
2005 |
4 |
15 |
101 |
452 |
2010 |
4 |
18 |
121 |
463 |
2015 |
4 |
25 |
125 |
477 |
Wilaya ya Mkuranga ina jumla ya Madiwani 35 kwa mchanganuo ufuatao:- Mbunge wa kuchaguliwa mmoja (1), Madiwani 25 wa kuchaguliwa na Madiwani 8 wa Viti Maalum.
Jedwali 2. Hali ya Watumishi kwa kipindi cha miaka sita (6)
MWAKA
|
MAHITAJI
|
WALIOPO
|
UPUNGUFU
|
2009
|
1513
|
1319
|
194
|
2010
|
2,057
|
1,644
|
413
|
2011
|
2,057
|
1,661
|
396
|
2012
|
2315
|
2014
|
301
|
2013
|
2353
|
2089
|
264
|
2014
|
2555
|
2302
|
253
|
2015
|
2929
|
2623
|
306
|
2016
|
3506
|
2719
|
787
|
SHUGHULI ZA KIUCHUMI ZA WAKAZI WA WILAYA YA MKURANGA.
Kilimo ni shughuli kuu ya kiuchumi kwa wananchi wa Wilaya ya Mkuranga. Inakadiriwa kuwa kiasi cha 85% ya wakazi wa Wilaya ya Mkuranga wanajishughulisha na Kilimo hususan kilimo cha Korosho, Nazi na aina mbalimbali za matunda kama mazao ya biashara. Kiasi cha wakazi waliobaki 15% hujishughulisha na shughuli nyingine zikiwemo, Uvuvi, Uvunaji wa mazao ya misitu, Biashara ndogo ndogo na ajira za ofisini.
Tofauti na mazao ya biashara, wakazi wa Wilaya ya Mkuranga hujishughulisha na kilimo cha mazao ya chakula kama vile Muhogo, Mpunga, Mahindi, Viazi vitamu na mazao ya jamii ya kunde.
2.1 HUDUMA ZA JAMII
Huduma za jamii zilizomo Wilayani ni pamoja na elimu iliyotolewa katika Shule za Msingi 116,(kati ya hizo Shule 111 ni za Serikali na 5 ni za binafsi). Shule za Sekondari 33, kati ya hizo 22 ni za Serikali na 11 ni za binafsi.Vituo 42 vya kutolea huduma ya Afya, na huduma ya usambazaji wa maji safi na salama inayotolewa katika vikao asilimia 54 ya wakazi wote wanaokadiriwa kufikia 223,573.Aidha, Kufikia mwezi Julai, 2015, huduma hizi za jamii bado zinatolewa kwa kiwango cha chini ya mahitaji kutokana na uwezo mdogo kifedha na miundo mbinu hafifu/duni iliyopo Wilayani hivi sasa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.