Tukielekea kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025, Mkuranga imebahatika kutembelewa na mjumbe wa Tume huru ya Uchaguzi Mhe. Balozi Omari Mapuri.
Akizungumza na wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya Wilaya Oktoba 24, 2025 katika ofisi ya Msimamizi wa uchaguzi Wilaya amesema anataka kuona Uchaguzi unafanyika vizuri na wenye kufuata Sheria, kanuni na taratibu ziliwekwa.
Amesema wasimamizi wote wanatakiwa kusimamia haki kwa kumtangaza mtu yoyote ambaye ameshinda kwa kura nyingi katika eneo husika la kupiga kura.
Aidha ameshukuru na kupongeza baada ya kusikia Mkuranga hadi sasa maandalizi ya Uchaguzi yanaendelea vizuri na kuwasihi wasimamizi husika kuendelea kusimamia haki na taratibu katika zoezi zima la Uchaguzi mpaka kukamilika kwake.
Mhe. Mapuri amefanya ziara hiyo kwa lengo la kujionea maandalizi ya Uchaguzi na anatarajia kuendelea na ziara hiyo Mkuranga Oktoba 25 hadi 26, 2025 kwa ajili ya kuona namna mafunzo kwa Wasimamizi na makarani yanavyoendeshwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.