KAZI/SHUGHULI ZA IDARA YA ELIMU SEKONDARI
1. Kurekebisha ikama ya Walimu ili kuboresha na kurahisisha utendaji kazi (ufundishaji) katika kuinua kiwango cha Taaluma.
2. Kusimamia, kufuatilia na kuwezesha Walimu kwenda likizo na upatikanaji wa nauli zao.
3. Kupanga mikakati ya utendaji na uwajibikaji katika kusimamia na kuinua kiwango cha taaluma kwa kufanya vikao na Wadau wa Elimu kama vile Wakuu wa Shule na Walimu.
4. Kusimamia na kuwezesha upatikanaji wa fedha za Ruzuku ya kuendeshea Shule pamoja na kufuatilia na kusimamia matumizi ya fedha hizo kwa kushirikiana na Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu.
5. Kuwezesha na kufuatilia upatikanaji wa gharama za mafunzo ya muda mrefu na muda mfupi kwa Walimu ili kuongeza kiwango cha ufanisi kazini.
6. Kufuatilia na kusimamia upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia Shuleni ili kuinua kiwango cha taaluma shuleni.
7. Kuwezesha upatikanaji wa gharama za chakula cha Wanafunzi shuleni kwa (Shule za Bweni).
8. Kusimamia na kufuatilia ufundishaji na ujifunzaji ili kuinua kiwango cha taaluma shuleni na ndani ya Halmashauri.
9. Kufuatilia na kusimamia uendeshaji wa Mitihani ya Kitaifa ya Kidato cha II, IV, na Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Ufundi ndani ya Wilaya.
10. Kufuatilia uendeshaji na ufanyikaji wa Mitihani ya ndani kama vile Mitihani ya utamilifu na Mitihani ya mihula.
11. Kuwezesha, kufuatilia na kusimamia ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali shuleni ili kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji katika Shule.
12. Kusimamia na kufuatilia upatikanaji wa samani mbalimbali Shuleni.
13. Kufuatilia na kuwezesha uboreshaji wa mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji ili yawe mazingira rafiki katika ufundishaji na ujifunzaji.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.