Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ali amekabidhi Magari pamoja na vyombo vingine vya usafiri vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1 zikiwa ni 10% ya mapato zinazotokana na makusanyo ya mapato ya ndani.
Magari hayo ameyakabidhi kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu Oktoba 16, 2025 katika viwanja vya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga.
Aidha amevitaka vikundi hivyo kuwa mabarozi wa kuwafikishia taarifa wengine kuwa tuna Serikali imara na sikivu ambayo inawawezesha kupata mikopo na kuwawezesha kufanya shughuli zao na kuongeza hali uchumi.
Amewataka kutunza vyombo hivyo na mikopo hiyo kwa kuilinda na kuitumia kulingana na miradi yao sambamba na kuzalisha ili kuweza kulipa na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati.
Akiongea kwa niaba ya wanufaika wa mikopo hiyo Salehe Bungala amesema wanamshukuru sana Mh, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kwa kuona umuhimu wa kuendelea kutoa mikopo hiyo kupitia Halmashauri kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kwani imeweza kuwakomboa kiuchumi lakini pia inaenda kuongeza ajira nyingine kwa watu wengine kupitia vyombo hivyo.
Awali akitoa salamu za Mh, Rais Mkuu wa Wilaya amewaambia wanufaika hao kuwa iko haja na umuhimu wa kumuenzi Rais kwa kuheshimu mikopo hiyo ya 10% ambayo huko nyuma ilithitishwa kwa lengo la kufanyia maboresho zaidi.
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga hutoa mikopo ya 10% mara nne kwa Mwaka.

Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.