Eneo la TEHAMA
1. Kuhakikisha mifumo ya TEHAMA iliyopo katika Halmashauri inafanya kazi kama inavyotakiwa;
2. Kutoa msaada wa kiufundi kwa watumishi wote wa Halmashauri katika eneo la TEHAMA;
3. Kutoa mafunzo kwa watumishi wa Halmashauri katika masuala ya TEHAMA zikiwemo programmu mbalimbali;
4. Kusimamia sera, mikakati na miongozo inayotolewa na Serikali Kuu juu ya uendeshaji wa mifumo, miundombinu na vifaa vya TEHAMA;
5. Kuibua mahitaji ya mifumo ili iweze kusanifiwa na kisha kutengenezwa na kutumika;
6. Kuchambua na kuainisha huduma zinazoweza kutolewa na mifumo ya kielekroniki katika Halmashauri;
7. Kuhakikisha miundombinu kiambo (Local Area Network) katika Halmashauri inafanya kazi na mtandao wa intaneti unapatikana;
8. Kuandaa mpango, bajeti, mpango kazi, mpango mkakati wa kuteleza kazi za TEHAMA katika Halmashauri;
9. Kutengeneza utaratibu mzuri wa kutunza taarifa na data ili ziweze kutumika wakati wa majanga;
10. Kufanya na kusimamia matengenezo ya vifaa vyote vya TEHAMA;
11. Kutafiti na kuchambua matatizo ya vifaa vya TEHAMA na kutoa suluhisho;
12. Kushirikiana kwa karibu na wataalamu wa TEHAMA wa Mkoa na wa Wizara ili kubadilisha uzoefu na kujengeana uwezo;
13. Kutoa specification za vifaa kwa ajili ya manunuzi;
14. Kushiriki katika zabuni za vifaa vya TEHAMA na kuhakiki ubora wake kabla havijaanza kutimika; na
15. Kuhakikisha Halmashauri ina tovuti na inapatikana wakati wote.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.