MAENDELEO YA JAMII
Kuelimisha, kuraghibisha na kufanya utetezi katika jamii, Kuwezesha jamii kiuchumi kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu, Kuelimisha na kuwazesha jamii kujua mahitaji na vipaumbele vyao kwa kuzitumia rasilimali zilizopo kwa kujiletea maendeleo, Kuelimisha na kushawishi jamii kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo, Kuwezesha uwepo wa usawa wa kijinsia, Kutambua makundi tete na kutoa msaada, Kuratibu shughuli za Asasi za Kiraia ikiwa ni pamoja na kuwezesha usajili wa Asasi hizo, Kuratibu shughuli za mapambano dhidi ya UKIMWI katika Halmashauri, Kufanya utetezi wa makundi tete katika jamii, Kutekeleza sera ya Maendeleo ya Jamii, Sera ya Jinsia na Sera ya Watoto, Kufafanua na kuelimisha jamii juu ya sera na sheria zinazosimamia makundi tete katika jamii, Kukusanya taarifa na tafiti mbalimbali zinazohusu maendeleo na ustawi wa jamii na kuzitumia/kutuma mamlaka za juu kwa utekelezaji zaidi, Kuhamasisha na kuratibu uanzishaji wa vikundi vya kijamii na uzalishaji mali katika jamii, Kuwezesha jamii kutambua vikwazo na fursa kwa maendeleo yao ili kuweza kuibua, kupanga pamoja na namna ya kusimamia/kutekeleza Miradi hiyo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.